Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/Stella Vuzo

Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo.

Sauti
3'3"
MONUSCO/TANZBATT-11

Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 watoa matibabu kwa raia nchini DRC

Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu ni Kapteni Fadhila Nayopa, Afisa habari wa kikosi hicho. 

Sauti
3'38"
UN News/Eugene Uwimana

Alice Nderitu: Dunia bado haijajifunza lolote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi

Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kuhakikisha asilani jinamizi hilo halitokei tena popote pale duniani.

Sauti
6'8"
© UNICEF/UN0560086/Gwenn Dubourthoumieu

Raia nchini DRC wasimulia jinsi wanavyonufaika na miradi iliyofanikishwa na MONUSCO

Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.

Miongoni mwa wanufaika ni shule ya msingi Lubumba hapa Kamanyola na Mwalimu Mkuu Texas Chekabiri anaelezea hali ilivyokuwa. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuelezea zaidi katika makala hii.

Sauti
3'4"
Unsplash/Dan Meyers

UNICEF na jitihada za kuimarisha huduma za Afya ya Akili kwa vijana nchini Rwanda

Makala hii inaeleza safari ya matumaini na uthabiti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNICEF Rwanda linaposhirikiana na Rwanda Biomedical Center (shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya) kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya akili kwa vijana. Katika mpango huu wa kutia moyo, UNICEF inavunja vizuizi na kukuza ujasiri kwa kutoa usaidizi muhimu kama vile nasaha shuleni

Sauti
2'54"
UNCTAD

UNCTAD, UNECA, Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara.

Sauti
3'8"
UNICEF VIDEO

Mradi wa maji warejesha matumaini kwa familia Wajir

Maji ni uhai, ni kauli mbiu ya miaka nenda rudi, lakini imesalia ndoto kwa wengi duniani hasa wakati huu mabadiliko ya tabianchi yanachochea ukame unaovuruga maisha ya binadamu, wanyama na mimea. Nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, iliyoko kaskazini-mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, uhaba wa maji ulisababisha familia kupoteza mifugo yao, mazao kukauka na ustawi wa jamii kutoweka.

Sauti
4'24"
UN News

Kituo cha malezi ya watoto nchini Kenya chatekeleza azma ya Umoja wa Mataifa

Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata ajira wamepata jawabu la changamoto wanazokumbana nazo pindi wakijifungua watoto wao. Changamoto kama vile mahali pa kumwacha mtoto kwa malezi ili aweze kuendelea na shule au kupata ajira. 

Sauti
7'35"