Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tuaminiwe tunapoanzisha mashirika - Suzan

Vijana tuaminiwe tunapoanzisha mashirika - Suzan

Pakua

Tarehe 12 mwezi huu wa Agosti dunia itaadhimisha siku ya Vijana duniani chini ya kauli mbiu Mshikamano wa vizazi: Kuunda Ulimwengu kwa Vizazi vyote, lengo likiwa kuhakikisha rika zote kwenye jamii zina mshikamano na vijana wanaweza kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kutafuta suluhu za changamoto katika jamii zinazowazunguka.

Kutoka nchini Tanzania Suzan Yumbe akiwa afisa Afya mkoani Mwanza aliamua kutumia elimu yake kuisaidia jamii kutafuta ufumbuzi wa magonjwa yanayoweza kusambaratishwa ikiwa jamii itapatiwa elimu ya afya ndio akaanzisha shirika la Afya Plus mkoani Iringa kwakushirikiana na vijana wenzie.

Lakini Suzan anasema, kuwa na wazo ni jambo moja na kuhakikisha linafanikiwa nisuala njingine na linahitaji usaidizi mkubwa katika jamii hususan zile ambazo haziamini kuwa vijana wanaweza kuleta suluhu za kudumu.

Leah Mushi amezungumza naye na anaanza kwa kueleza kilichomsukuma kuanzisha shirika la AfyaPlus.

Audio Credit
Anold kayanda/ Leah Mushi
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
Leah Mushi