Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji ni uhai na yanabadili maisha ya watu na jamii zao:UNCDF

Maji ni uhai na yanabadili maisha ya watu na jamii zao:UNCDF

Pakua

Mradi wa nishati ya maji wa  AHEPO upo katika kijiji cha  Lifakara kwenye maporomoko ya Mbangamao kwenye mto  Mtandasi wilayani Mbinga mkoani , Ruvuma Kusini mwa Tanzania.

Mradi huo ambao unafadhiliwa na shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa UNCDF unalenga sio tu kuwapunguzia adha wananchi wa wilaya hiyo bali pia kubadili kabisha maisha yao ya kiuchumia na kijamii kwa kuwapata nishati mbadala kwani fursa ya nishati ni kitovu cha maendeleo ya jamii yoyote na ni moja ya mambo ya lazima katika kukidhi mahitaji muhimu na ya msingi ya binadamu.

Bila fursa ya mahitaji ya msingi ya nishati mathalani ya kupikia, taa, usafiri na mawasiliano  watu wengi na husuan wanake wanatumia muda mwingi na nguvu katika shughuli za kukidhi mahitaji hayo. 

Tuungane na Happiness Palangyo katika makala hii kuhusu mradi huo.

Audio Credit
Leah Mushi / Hapiness Palangyo
Audio Duration
4'56"
Photo Credit
UNCDF/Video