Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Changamoto wanazokumbana nazo wahamiaji zaangaziwa

Vijana, wake kwa waume hukimbia makwao kutokana na usalama au kusaka maisha bora na wakati mwingi hukumbana na changamoto nyingi wakati wakitafuta hifadhi katika nchi zingine haswa zilizostawi.

Licha ya kwamba changamoto ni nyingi lakini kambi za muda wanayowekwa wahamiaji hawa kila uchao hupkea watu wapya je ni yapi wanayowakumba wahamiaji hawa basi ungana na Grace Kaneiya katika ripoti ifuatayo.

Juhudi za kupambana na ukimwi zamulikwa nchini Burundi na Tanzania

Mnamo Alhamisi wiki hii, Kongamano la ngazi ya juu limefanyika huko Washington DC likiangazia vichocheo vya kijamii vinavyoweza kusaidia kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri.

Katika kongamanohiloambalo lilijumuisha Benki ya Dunia, Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP na Shirika linalokabiliana na Ukimwi, UNAIDS, Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Michel Sidibé alisema kuwa  mabilioni ya dola yanayoelekezwa kwenye sekta hiyo hayawezi kuwa na ufanisi pekee bila kufanyika mabadiliko.

Onesho la ubunifu wa mitindo ya mavazi lafanyika UM

Ukifikiria Umoja wa Mataifa hapana shaka unawaza juu ya jamii mbalimbali, tamaduni zao na tofuti zao zikiwa pamoja katika taasisi hii ya kimataifa. Na pia hapana shaka unawaza kuhusu masuala ya kisiasa na diplomasia ya kimataifa.

Sio rahisi kuwaza kuhusu maonesho ya ubunifu wa mitindo ya mavazi katika Umoja huo. Kulikoni? Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo itakayokueleza yaliyojiri humo.

Mradi mpya katika kukabilina na utapiamlo Niger ni wa kutumainisha

Utapiamlo ni janga la kitaifa nchini Niger na unaathiri mamia ya maelfu ya watoto.

Ni janga ,ambalo UNICEF na wadau wanajaribu kukabilina nalo kufuatia mradi bunifu wa kutoa mafunzo kwa akina mama kuweza kupima utapiamlo.

Mradi huu unalenga kuhakikisha kwamba utapiamlo unanaswa na kutibiwa kabla ya kusababaihsa maafa basi ungana na Grace Kaneiya katika ripoti

Wakimbizi wa Sudan Kusini wamiminika Kenya na Uganda

Mapigano nchini Sudan Kusini yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wanaowasili katika nchi jirani kutafuta usalama. Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Kambi ya Kakuma Kaskazini Mashariki mwa Kenya imekuwa ikipokea wakimbizi wapatao 300 kila siku, huku idadi ya wakimbizi wanaowasili nchini Uganda kwenye kambi ya Kiryandongo ikiwa imepanda pia. John Kibego wa Redio washirika ya Spice FM yupo kwenye kambi hiyo na amefanya mahojiano maaluma na Joseph Msami kuhusu kile anachokiona kamabini hapo.

(Sauti Maojiano)

MONUSCO yatoa usaidizi kwa wapiganaji waliojisalimisha DRC

Zoezi la usaidizi kwa wapiganaji wanaojisalimisha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC linaendelea ambapo wapiganaji hao wanajumuishwa katika jamii huku wengine wakijumuishwa katika jeshi la serikali kwa hiari.

Joseph Msami anamulika zoezi hili huko mashariki mwa DRC katika makala inayoangazia namna ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC unavyosaidia kuweka utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa na mizozo kwa miongo kadhaa.

Usawa wa kijinsia wamulikwa nchini Tanzania

Mwaka 2000 wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha malengo ya maendeleo ya Milenia, malengo yako manane na lengo namba Tatu ndiyo mada kuu ya Makala yetu wiki hii.Lengo hilo ni kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake. Masuala yanayomulikwa hapa ni kuondoa tofauti ya uandikishaji watoto wa kike na kiume mashuleni, uwiano wa ajira nje ya sekta ya kilimo na tatu ni ushiriki wa wanawake kwenye maamuzi ikiwemo kuingia katika mabunge na kushika nafasi za kisiasa. Miongoni mwa nchi zilizoridhia malengo hayo ni Tanzania.