Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Madhara ya matumizi ya bidhaa za tumbaku

Matumizi ya bidhaa za tumbaku kwa mfano uvutaji wa sigara una madahara chungu nzima kiafya amabayo hupelekea madhara yanayo mgharimu hela nyingi katika kutafuta matibabu mtu anyetumia bidhaa hizo basi katika makala ifuatayo Salim Chiro wa radio washirika pwani fm anaangazia swala hilo ungana naye.

Udhibiti wa madawa ya kulevya Tanzania

Mkutano wa udhibiti wa madawa ya kulevya umemalizika hivi karibuni mjiniViennaAustriaambapo wakuu wa nchi na mashirika mbalimbali walijadili mbinu za kukabiliana na utenegezaji na usambazaji wa madawa hayo haramu.

Mkutano huo umefanyika wakati Umoja wa Mataifa kupitia shirikalakekudhibitiuhalifu na madawa ya kulevya UNODC likisema kuwa utengenezaji, usafirishaji na matumizi ya madawa hayo unaendelea kusababisha hatari kubwa kwa afya za watu kila mahali ukiathiri maendeleo endelevu ya nchi na kanda mbalimbali.

Jeshi la Somalia laendesha operesheni ya kuwasaka Al shabaab

Mfululizo wa matukio ya kigaidi yameendelea kuripotiwa nchini Somalia likiwemo la hivi karibuni zaidi ambapo wazee wa nane wa koo nchini humo waliuwawa huku kundi la kigaidi la Al shabaab likikiri kuhusika katika tukio hilo.

Jeshi la Somalia kwa kushirikiana na vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM liko katika operesheni kali ya kutokomeza mtandao wa kundi hilo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

UNHCR yazungumzia kuzama kwa wakimbizi wa DRC huko Uganda

Taarifa za kuzama kwa boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliokuwepo kwenye kambi ya Kyangwali nchini Uganda imeibua simanzi huku Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, ukieleza kuhuzunika na kushtushwa na taarifa hizo. Boti hiyo ikiwa na mamia ya wakimbizi hao wakiwemo watoto ilizama Jumamosi kwenye Ziwa Albert. John Kibego wa Radio washirika Spice FM alizungumza kwa njia ya simu na Andrew Mbogori, afisa wa UNHCR ambaye amekuwa kwenye harakati za kusaka miili.

CSW58 yafunga pazia: Shina Inc. yapigia chepuo ubia na elimu kwa jamii kuhusu tamaduni

Baada ya takribani wiki mbili za vikao kuhusu hali ya wanawake duniani na mustakhbali wa kundi hilo baada ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo mwakani na ajenda ya maendeleo endelevu inayofuatia, washiriki wamekuwa na maoni kuhusu mkutano huo uliokutanisha wanawake, wanaume na vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoi mwao ni Jessica Kamala-Mushala kutoka shirika lisilo lakiserikali la Shina linalolenga kukomboa makundi yaliyo hatarini ikiwemo wanawake, vijana na watoto.

Wabunge wanawake kutoka Kenya wasema wanataka usawa wa kijinsia katika uongozi

Mkutano unaoangazia hali ya mwanamke CSW ukiwa unafikia kilele chake leo mjiniNew York, wanawake wabunge kutokaKenyawamesema moja ya changamoto kubwa ambayo nchiyaoinakabiliwa ni kuongezeka kwa nafasi ya wanawake katika maamuzi kwa kuwashirikisha katika vyombo vya kisiasa pamoja na utamaduni unaokandamiza kundihilo.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii wanawake hao wanaowakilisha taasisi ya wanawake wabunge nchiniKenyawameelezea hatua watakazochukua ili kuleta mabadiliko. Ungana na Joseph Msami katika mahojiano hayo.

Ugonjwa wa Kifua Kikuu waangaziwa nchini Kenya

Machi 24 ni siku ya kifua kikuu duniani. Siku hii imetengwa kwa ajili ya kuhamashisha na kuleta uelewa kuhusu mzigo wa kifua kikuu na jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Fikia watu hao milioni 3”. Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba ijapokuwa ugonjwa wa kifua kikuu unatiba lakini theluthi moja ya watu milioni tisa ambao huugua ugonjwa huo hawapati tiba.

Mradi wa EXPAND-TB waleta nuru katika vita dhidi ya Kifua Kikuu Tanzania: Dkt. Mleoh

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu duniani tarehe 24 mwezi huu, nchini Tanzania harakati za kupambana na ugonjwa huo ikiwemo Kifua Kikuu sugu zinaanza kuzaa matunda. Nuru hiyo inatokana na mradi wa shirika la afya duniani, WHO unaolenga nchi 27 ikiwemo Tanzania ambako Kifua Kikuu Sugu kinahatarisha afya ya umma. Je mradi huo umefanya nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Dokta Liberate Mleoh, Naibu Meneja wa Mradi wa Kitaifa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini humo ambaye anaanza kwa kuelezea hali ya ugonjwa huo Tanzania.

Makabila asilia yapaza sauti New York

Mkutano wa hali ya wanawake CSW ukiendelea mjini New York makabila asilia yanazidi kupaza sauti zao kuhusu haki zao za kimsingi matahalani elimu, na huduma nyingine za kijamii.

Akiwa mitaani mjini humo Joseoph Msami wa idhaa hii amekutana na miongoni mmoja wa wamasai kutoka nchiniTanzania, ungana naye

Usafi wa sikio waangaziwa

Usafi na utunzaji wa sikio ni suala muhimu sana katika afya ya binadamu kwani kwa mara nyingi watu hawana habari sahihi kuhusu namna ya kutunza au kusafisha sikio. basi ungana na John Kibego wa Radio washirika spice Fm nchini Uganda katika ripoti ifuatayo.