Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wasomali wafurahia Kombe la Dunia, kinyume na 2010

Nchini Somalia, vikosi vya kulinda amani vya AMISOM pamoja na serikali ya Somalia, zinajitahidi kulinda utulivu katika mitaa ya Mogadishu, usiku na mchana, ili watu waweze kufurahia kombe la dunia.

Wakati wa kombe la dunia lililochezwa Afrika Kusini, wanamgambo wa Al-Shabab walikatalia watu kuangalia mechi kwenye televisheni zao binafsi ama za migahawa. Sehemu nyingi zilifungwa. Mwaka huu hali ikoje? Basi Ungana na Priscilla Lecomte katika makala hii.

Baraza la Mazingira latamatishwa na matumaini

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mazingira duniani  umefanyika wiki hii huko Nairobi Kenya, maudhui ya jumla yakiwa ni malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa chombo hicho kilichoundwa kufuatia mkutano wa Rio +20 nchini Brazili mwezi Juni mwaka 2012 wa kutaka kuanzishwa kwa mamlaka simamizi ya shirika la mazinigira duniani, UNEP.

Makundi kinzani Somalia yatia saini makubaliano ya mamlaka za mpito za majimbo

Nchini Somalia, uchaguzi mkuu utafanyika mwaka 2016, na kinachofanyika sasa ni mchakato wa kisiasa utakaowezesha kuundwa kwa serikali shirikishi za majimbo kama njia ya kuwezesha kufanikisha uchaguzi huo.

Hatua ya kipekee imefikiwa wiki hii nchini humo kwa makundi mawili kinzani Kusini magharibi ya SW-3 na SW6 kutia saini ya kujiunga na mamlaka ya mpito ya ukanda wao ikijumuisha mikoa mitatu.

Je mapokeo ya hatua hiyo ilikuwaje? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Baharia amekuletea nini?:IMO

Siku ya mabaharia duniani imeadhimishwa kwa kutambua mchango wa kundi hilo katika maisha ya kila siku ya jamii nzima duniani. Shirika la Kimataifa la masuala ya bahari, IMO limetumia siku hiyo kwa kutoa wito kwa watu kutafakari mchango wa mabaharia katika shughuli wanazofanya kila siku na vitu wanavyovitumia kila siku.

Je nini muktadha wa maudhui hayo, Naibu Mkurugenzi wa IMO Juvenal Shiundu amefafanua katika mahojiano na Amina Hassan wa Idhaa hii na hapa anaanza kwa kuelezea umuhimu wa siku hii kwa mabaharia …….

Ufugaji wakwamua maisha ya wajane

Katika maeneo ya Bonde la Ufa, wakazi hufuga wanyama, ngombe, mbuzi kondoo na hata punda kama njia ya kujiendeleza na kujikimu maishani. Leo tunangazia juhudi za akina mama waliofiwa na waume wao ambao wanajitegemea kwa njia hii.

Basi jiunge na John Ronoh kwa makala hii….

UNHCR yasaidia wakimbizi wa ndani Iraq

Wiki iliyopita, mauaji yalitokea nchini Iraq, maeno ya Mosul, baada ya kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali cha ISIL kukamata mji huo. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, zaidi ya raia 500,000 walikimbia Mosul na kuacha mali zao ghafla, kwenda kutafuta hifadhi katika maeneo ya Kurdistan, kaskazini mwa Iraq, UNHCR na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yakijitahidi kuwapatia hifadhi na misaada ya awali. Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii!

FAO yatunza msitu wa Mau, Kenya na jamii yake

Nchini Kenya, sehemu za misitu zinafunika asilimia 1.9% tu ya ardhi, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, ambayo ni idadi ndogo sana ikilinganisha na asilimia 68 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kutunza na kupanda upya msitu wa Mau, nchini humo, kumekuwa jambo la msingi ili kuzuia jangwa kubwa la kiekolojia. Lakini utunzaji wa msitu huo uliibua changamoto nyingine, zikiwemo kusaidia jamii ya watu wa asili wa Ogyek, ambao walikuwa wanategemea msitu tu kwa kuishi.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii!

Kilimo cha mpunga chaboreshwa Zanzibar kupitia nguvu za kiatomiki

Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, linatumia miyonzi ya nyuklia kuboresha mbegu za mazao mbalimbali na kuimarisha kilimo katika nchi zinazoendelea.

Mbegu hizo bora zinasaidia kustahimili ukame na wadudu mbalimbali na kuongeza mavuno ya mazao hayo. mfumo huo umeleta mabadiliko makubkwa kwenye jamii ya wakulima, katika wilaya ya Kaskazini A, kisiwani cha Zanzibar, Tanzania. Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hiyo!

UN Photo/Paulo Filgueiras

Wananchi wanataka uwajibikaji wa viongozi, na ni haki yao: Dkt. Asha-Rose

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefanya mjadala wa ngazi ya juu kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa kisheria kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Miongoni mwa watoa mada alikuwa Dkt. Asha-Rose Migiro Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba wa Tanzania na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa  Mataifa. Punde baada ya kutoa mada Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa alimuuliza kwa kina suala la haki za binadamu  na hapa Dkt, Asha-Rose anaanza kuelezea ujumbe wake.