Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Elimu Tanzania yakabiliwa na changamoto

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kuhusu elimu kwa wote ambalo ni lengo namba mbili la Milenia, imebaini kuwa kasoro katika sekta ya elimu hugharimu serikali duniani kote dola Bilioni 129 kwa mwaka. Hii ni kwasababu asilimia 10 ya fedha zinazoelekezwa kwenye elimu ya msingi hupotelea kwenye kiwango duni cha elimu ambacho hakiwawezeshi watoto kufuta ujinga wa kutokujua kusoma.

Mimba na ndoa za utotoni kupingwa kwa marathoni Jumapili

Nchini Tanzania Jumapili hii kutafanyika mbio za kimataifa za  marathoni za Kilimanjaro Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu, UNFPA  itatumia mbio hizo kueneza ujumbe wa kupinga mimba na ndoa za utotoni.

Katika mahojiano Afisa wa UNFPA Sawiche Wamunza  amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo kuwa hii ni mara ya pili wanadhamini mbio hizo na wanaamini ni njia muhimu ya kuwafikia vijana kwenye nchi hiyo ambayo asilimia 23 ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wamepata watoto wakiwa na umri mdogo.

Onyesho la filamu ya miaka 12 utumwani yafungua maadhimisho ya biashara ya utumwa atlantiki

Maadhimisho ya siku ya utumwa na biashara ya utumwa huadhimishwa kila mwaka Machi 25. Katika kuanza kumbukumbu ya maadhimisho ya mwaka huu yalifunguliwa rasmi na onyesho la filamu Miaka 12 utumwani ambayo mmoja wa waigizaji ni Lupita Nyon'go kutoka Kenya.

Onyesho hilo lilifanyika jioni ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na Grace Kaneiya alikuwa shuhuda wetu basi ungana naye katika makala ifuatayo.

Uwezo wa kusoma bado ni ndoto kwa wengi

Hivi karibuni shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO lilichapisha taarifa iliyoanisha hali ya elimu ya msingi duniani ambapo pamoja na mambo mengine ripoti hiyo inaonyesha kuwa kati ya vijana wanne mmoja hajui kusoma duniani kutokana na ukweli kwamba elimu hiyo ya msingi haijatekelezwa kwa nchi nyingi kama inavyopaswa.

Noel Thomson wa radio washirika Afrya radio ya Mwanza Tanzania amefuatilia suala hilo na kuandaa taarifa ifuatayo.

Lugha ya mama ina umuhimu katika kuinua kiwango cha elimu

Februari 21 ni siku ya lugha ya mama duniani, siku hii huadhimishwa kusherehekea uwepo wa lugha nyingi na tamaduni tofauti kote ulimwenguni. Lugha ya mama ni lugha ya kwanza imtokayo mtu pale anapoanza kuwa na uwezo wa kuzungumza. Mtu anaweza kuwa ni raia wa Uganda na kabila lake ni muankole, lakini akazaliwa Marekani na iwapo lugha ya kwanza kuifahamu ni Kiingereza basi hiyo inakuwa ndiyo lugha ya mama kwake yeye.

Siku hii ilianzishwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika kuimarisha , kudumisha na kulinda lugha zote zinazotumika na watu tofauti duniani.

Malala atembelea kambi ya wakimbizi wa Syria

Huku mzozo wa Syria ukiendelea, wananchi wanakimbilia nchini jirani kutafuta hifadhi. Mmjoa ya nchi hizo ni Jordan ambako wakimbizi wanawasili kwa mamia. wengi wamesikia kuhusu mzozo na masaibu wanayokumbana nayo wakimbizi na pia kuna baadhi ya watu ambao wamepata fursa ya kujionea hali halisi mmoja wa shuhuda ni mtoto Malala Yousfzai.

Basi ungana na Grace Kaneiya katika ripoti ifuatayo

Mafunzo kwa jeshi, ishara ya kuimarika kwa nchi: Somalia

Wakati taifa la Somalia likiwa linajimarisha katika nyanja mbalimbali ujenzi wa taifa hilo unahusisha sekta ya ulinzi ambapo mkakati wa hivi karibuni zaidi ni mafunzo kwa jeshi hilo mafunzo yanayofanywa chini ya uratibu wa vikosi vya muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM.

Ungana na Joseph Msami katika ripoti ifuatayo

Mbwa watumika kumiarisha ulinzi kwa raia Sudani Kusini

Wakati hali ya machafuko ikiendelea nchini Sudani Kusini ulinzi hususani kwa raia ni changamoto kubwa kwa sasa. Umoja wa Mataifa ambao licha ya juhudi ambazo unachukua kuhakikisha machafuko yanakomeshwa unachukua hatua stahiki za ulinzi na sasa wanyama mbwa wanatuika wka ajili ya ulinzi nchini humo.

Ungana na Joseph Msami katika ripoti inayofafanua zaidi