Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

FAO na kaulimbiu "Samaki safi, maisha bora"

Uvuvi wa kupindukia ni moja ya tishio kubwa kwa utunzaji wa rasilimali za mabahari na usalama endelevu wa chakula. Shirika la chakula na Kilimo Duniani FAO limejadili changamoto hiyo katika kongamano la kimataifa kuhusu bahari na usalama wa chakula, lililofanyika The Hague, Uholanzi, kuanzia tarehe 24 hadi 25, April mwaka huu. Kwa mujibu wa FAO, ni muhimu kuelimisha jamii kuhusu uvuvi endelevu kwanzia ngazi ya wavuvi wadogo wadogo wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya rasimali hiyo.

Filamu zaendelea kuleta msisimko lakini wabunifu mashakani:WIPO

Ulimwengu unaadhimisha siku ya hakimiliki duniani tarehe 26 Aprili, maudhui ni Filamu: Msisimko wa dunia! Shirika la hakimiliki duniani, WIPO linasema filamu miaka nenda miaka rudi zimesaidia jamii kujifunza mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa na hata wakati mwingine kuwafikisha watazamaji maeneo ambayo hawajafika. WIPO inatoa pongezi kwa wabunifu wa filamu hizo na washiriki lakini wakitoa angalizo kuwa mwelekeo wa uwepo wa kazi hizo uko mashakani kwani teknolojia pamoja na kusaidia kuboresha filamu, inawezesha kutazamwa bila malipo na kukiukwa suala la hakimiliki bunifu.

Ongezeko la gesi joto ni kutoitendea haki dunia:Muyungi

Ni lazima wanadamu waitendee haki dunia kwa kuwa hakuna dunia nyingine na njia pekee ni kuhakikisha ukomeshwaji wa ongezeko la gesi joto. Huu ni wito wa wake mwenyekiti wa kamati ya dunia ya kisayansi na taaluma ya makataba kuhusu makubaliano ya hali ya hewa Richard Muyungi akizungumza katika siku ya kimataifa ya sayari dunia

Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa idhaa hii Muyungi aliyebobea katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi anasema ujenzi wa miji na vijiji usioongeza joto ni muhimu . Anaanza kueleza wito wake katika kuadhimisha siku hii.

Harakati za kupambana na Malaria na changamoto zinazoibuka Mwanza Tanzania

Wakati dunia inaelekea kuadhimisha siku ya Malaria duniani tarehe 25 mwezi huu, ripoti za shirika la afya duniani, WHO zinasema kuwa kiwango cha vifo vitokanavyo na Malaria duniani kimepungua kwa asilimia 48 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuanzia mwaka 2000 hadi 2012. Halikadhalika vifo vimepungua kwa asilimia 42 kwa makundi yote. Sababu mojawapo inayotajwa kupunguza vifo ni matumizi ya vyandarua vilivyotiwa VIUATILIFU na upuliziaji wa dawa majumbani.

UNMISS yaboresha vipato vya wananchi Sudani Kusini

Wakati machafuko nchini Sudani Kusini yakiripotiwa kundelea ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS umeanzisha mradi wa kusafisha magari ambao angalu utaleta matumaini ya kipato katikati ya ghasia zilizosababisha hali tete ya usalama wa chakula kutokana na shughuli za kiuchumi kudidimia.

Ungana na Joseph Msami katika makala inayosimulia namna mardi huu unavyotekelezwa.