Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

22 Januari 2020

Hii leo tunaanza na kauli ya Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa kuhusu changamoto 4 na suluhu 4 kwa ajili ya kuhakikisha mafanikio ya karne ya 21 hayafutiliwi mbali kisha tunakwenda Kigoma kumulika jinsi miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye kilimo inavyoendelea kufuta kilimo cha "tangulia nakuja" hususan wilayani Kibondo, tumezungumza na Martine Kapaya.

Sauti
13'34"

21 JANUARI 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutokomeza Ukimwi, UNAIDS limesema afya bora si haki ya matajiri pekee, bali kila mtu. Jukwaa la kidijitali kukusanya takwimu kuhusu njaa na mzozo duniani lazinduliwa. Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock amesema Umoja wa Mataifa utafanya kila uwezalo kuwasaidia wakimbizi Za’atari. 

Sauti
9'54"

20 JANUARI 2020

Kigori 1 kati ya 3 kutoka familia maskini hawajawai kwenda shule limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Mangariba watupa visu vya ukeketaji huko Sierra Leone.  Uvutaji tumbaku unaongeza hatari ya madhila baada ya upasuaji limeonya shirika la afya duniani WHO. 

Sauti
10'53"

16 JANUARI 2020

Katika Jarifada la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Watu milioni 45 katika nchi 16 za Kusini mwa Afrika maisha yao yako hatarini kutokana na njaa, na hatua za haraka za msaada zinahitajika limesema shirika la Umoja wa Matafa la mpango wa chakula duniani WFP

-Kimbunga Idai kilifungua macho ya madhila yanayowasibu watu wenye ulemavu nchini Zimbawe kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na elimu, UNESCO

Sauti
11'44"

14 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea 

-Dola milioni 477 zahitajika ili kunusuru maisha ya takriban watu laki tisa nchini Sudan kwa mahitaji ya kibinadamu kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lililozindua ombi hilo leo mjini Khartoum 

-Ofisi ya miradi ya Umoja wa Mataifa, UNOPS kwa kushirikiana na Benki ya dunia pamoja na wadau wenyeji, wanafanya juhudi za kuboresha huduma mijini pamoja na nishati ya umeme kwa mamilioni ya watu wa Yemen.

Sauti
10'41"

13 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Miaka 10 baada ya tetemeko baya la ardhi nchini Haiti athari zake zinaendelea kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM

-Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeutenga mwaka 2020 kuwa ni wa afya ya mimea kwa kutambua mchango na thamani ya mimea hiyo kwa maisha ya watu na syari dunia

-Maelfu ya Wavenezuela wakiwemo watoto wanaendelea kufungasha virago na kukimbilia nchi jirani ikiwemo Brazil limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF

Sauti
11'50"

10 JANUARI 2020

Flora Nducha wa UN News Kiswahili anatupa habari zifuatazo:

-Ripoti ya Umoja wa Mataifa yaonya yaliyojiri baina ya Walendu na Wahema DRC huenda ukawa uhalifu dhidi ya ubinadamu 

-Kwa mujibu wa UNCTAD uwekezaji kutoka pato la taifa ni hatua ya kwanza katika kufanikisha SDGs Afrika

-Mahitaji ya upinzani Lirangu Sudan Kusini yamenza kutimizwa kwa mujibu wa UNMISS

-Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC hii leo imelitunukia tuzo ya juu ya kikombe cha  Olimpiki shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR 

Sauti
10'37"

09 JANUARI 2020

Katika Jarida letu la Habari hii leo Arnold Kayanda anakuletea 

-UNHCR yatoa changamoto kwa Muungano wa Ulaya kuufanya mwaka 2020 kuwa wa ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji

-Kuanza tena kwa doria inayojumuisha mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSCA ni neema na amani kwa raia 

-Nchini Burkina Fasso mradi wa pamoja wa shirika la chakula na kilimo FAO, Muungano wa afrika Au na serikali ya nchi hiyo kupambana na hali ya jangwa umeleta tija kwa wananchi

Sauti
11'45"

08 JANUARI 2020

katika jarida la habari la umoja wa mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katika mkuu aisihi Ghuba kujizuia na machafuko zaidi na kuanza majadiliano

-Shirika la Afya Duniani WHO lahaha kusaka ufadhili kunisuru maelfu na ugonjwa wa surua nchini DRC

-Machafulo Burkina Fasso yawakosesha elimu maelfu ya watoto lasema shirika la UNICEF

-Makala yetu hii leo yatupeleka Kenya kwa kijana aliyekuwa mhalifu sugu lakini sasa kabidili maisha yake na ya wengine 

Sauti
11'38"

07 Januari 2020

Mradi wa afya wa Benki ya dunia, mkombozi kwa maeneo ya pembezoni, Afghanstan.  OCHA inasikitishwa na hali inayoendelea kuzorota Idlib, Syria. Ghasia West Darfur, Sudan zimewaathiri maelfu. 

Sauti
10'25"