Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

06 MACHI 2020

Katika Jarida letu leo la mada kwa kicha Grace Kaneiya anakuletea

Miaka 25 baada ya jukwaa la Beijing la kuchukua hatua kuhusu Haki za wanawake, Umoja wa Mataifa unasema wakati ni sasa na hakuna kinachohalalisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeona zaidi ya dola milioni 260 kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wa DRC walioko nje na jamii zinazowahifadhi

Sauti
11'58"

05 MACHI 2020

GRACE: Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

 

JINGLE (04”)     

 

GRACE : Ni Alhamisi ya Machi nne mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi GRACE KANEIYA

 

1: Elimu kwa wasichana haina maana iwapo jamii ina mtazamo hasi dhidi yao- Ripoti

Sauti
12'58"

04 MACHI 2020

Elimu kwa wasichana haina maana iwapo jamii ina mtazamo hasi dhidi yao imesema ripoti ya mashirika ya Umoja wa Mataifa. Virusi vya Corona vyasababisha kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa CSW. Tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia waathirika wa vita Idlib imesema WFP.

Sauti
11'28"

03 MACHI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Anold Kayanda anakuletea 

-Umoja wa Mataifana washirika wake leo wamezindua ombi la pamoja la kuchangisha dola milioni 877 ili kushughulikia janga la wakimbizi wa Rohingya na jamii zinazowahifadhi nchini Bangladesh.

-Mlo shuleni umeelezwa kuwa ni kichocheo cha maendeleo na ukuaji uchumi  Barani Afrika na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.

Sauti
11'13"

02 MACHI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi kuhusu machafuko nchini Syria imesema miaka karibu tisa tangu kuanza kwa vita hivyo sasa hali inakuwa janga kubwa la kibinadamu huku maelfu ya wanawake, watoto na wanaumme wakiendelea kubeba gharama

Sauti
11'38"

28 Februari 2020

Hakuna mgonjwa mpya wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika siku 7 zilizopita, ni moja  ya habari muhimu hii leo kwenye muhtsasari wa habari na kisha ni mada kwa kina leo tukijikita huko wilayani Bukoba mkoa wa Kagera nchini Tanzania, mwandishi wa Radio washirika ya Kasibante FM Nicolaus Ngaiza anazungumza na mkunga wa jadi. Neno la Wiki leo ni gidamu, wafahamu maana yake? Tumekwenda BAKIZA huko Zanzibar! Basi  ungana na  mwenyeji wako hii leo jaridani, Flora Nducha.

Sauti
9'41"

27 Februari 2020

Suala la matumizi ya bidhaa za uraibu kama vile pombe na madawa ya  kulevya miongoni mwa watoto ni kipaumbele cha ripoti mpya ya Bodi  ya udhibiti wa madawa ya kulevya duniani, ripoti ambayo imetolewa leo huko Vienna, Austria na ndio miongoni mwa taarifa zetu hii leo, bila kusahau apu mpya ya kusaidia mtu kutumia kwa faragha taarifa zake binafsi mtandaoni na pia tunabisha hodi Ujerumani kwa mkimbizi wa Syria ambaye baada ya kupitia machungu hii leo anapika vyakula na kuuzia watu kadhaa mashuhuri akiwemo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Sauti
9'56"

26 Februari 2020

Nchi kushindwa kuwasilisha taarifa zao kuhusu virusi vya Corona, ni changamoto kubwa katika kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo hatari, yasema WHO. Huko Nzara nchini Sudan  Kusini moto wa nyika waleta tafrani kubwa na nchini Mali, rubani wa ndege za kivita kutoka El Salvador asihi wanawake wajitokeza. Katika makala leo Saa Zumo kutoka radio washirika Pangani FM mkoani Tanga  nchini Tanzania azungumza na muuguzi mkunga mwanaume na mashinani tunarejea tena Syria, kunani? Basi ungana na Flora Nducha.

Sauti
12'12"

25 Februari 2020

Jaridani hii leo Flora Nducha anaanza na uzinduzi wa jopo la kusimamia masuala ya watu kufurushwa makwao, uzinduzi umefanyika Geneva, Uswisi kisha tunabisha hodi Chad ambako watu wamefurushwa na kukimbilia Darfur nchini Sudan. Nchini Myanmar mradi wa ILO waleta nuru kwa wafanyakazi wa viwanda vya kushona nguo na mabegi na makala ni mwendelezo wa masuala ya wakunga na wauguzi na mashinani tunamsikia mtoto mkimbizi wa ndani nchini Syria akisema kile afanyacho, kuuza maua ili kulisha familia yake. Karibu!

Sauti
11'47"

24 FEBRUARI 2020

Jaridani Flora Nducha leo Februari 24, 2020

-Guterres azindua wito wa kuchukua hatua ili kulinda haki za binadamu duniani

- Vitisho dhidi ya haki za binadamu vinaongezeka lakini pia suluhisho-Bachelet

-Wakimbizi wanaokimbia ukatili wapata kimbilio kupitia chifu mji wa Kaya, Burkina Faso

Kwenye makala tunaeleka nchini Uganda.

Audio Duration
12'1"