Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

20 Disemba

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo , Grace Kaneiya anakuletea

-Uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waahirishwa kwa wiki moja zaidi, huku mkuu wa mahakama ya ICC akionya uhalifu dhidi ya ubinadamu kuwajibishwa

-FAO yawainua wakulima wadogowadogo nchini Tanzania kwa kuwapatia stadi za kilimo

-Msichana mkimbizi kutoka kambi ya Dadaab nchini Kenya aoongoza kwa alama za juu katika kuhitimu elimu ya msingi

-Makala leo inamulika afya kwa wote nchini Burundi

Sauti
13'12"
UNICEF/Vincent Tremeau

Wakimbizi wa ndani DRC wafarijika kwa kusaidiana:UNHCR

Wakati machafuko yakiendelea kusambaratisha familia na kuwalazimisha kufungasha virago nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC maelfu ya wakimbizi wa ndani wanatafuta faraja kwa kusaidiana  kupitia ushirika ulioanzishwa kwa minajili ya kuchagiza ulinzi wa haki za binadamu na kusaka suluhu ya changamoto zinazowakabili 

Sauti
2'2"

19 Disemba 2018

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Arnold Kayanda anaangazia

-Usafiri wa mabasi ya abiria maarufu kama "matatu" nchini Kenya ulivyo hatari kwa afya na mazingira kwa mujibu wa UNEP

-Wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wapata faraja kwa kusaidia

-Huko kambini Kakuma nchi Kenya wakimbizi wanasema msitusahau nasi " Kakuma tuna vipaji"

-Makala leo inatupeleka Morogoro Tanzania kwa kijana mchonga vinyago anaeleza kwa nini sanaa hiyo imekuwa mtihani siku hizi

Sauti
11'52"
UN / Evan Schneider

Harakati za Rebeca Gyumi za kumkomboa mtoto wa kike Tanzania zatambuliwa UN

Washindi wa tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa  Mataifa kwa mwaka 2018 hii leo wamepatiwa tuzo hizo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani.

Washindi hao ambao ni watu watatu na shirika moja, wamekabidhiwa tuzo hizo wakati wa kikao cha 58 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichoongozwa na Rais wa Baraza hilo Maria Fernanda Espinosa.

Bi.Espinosa ndiye amefungua kikao hicho ambapo kabla ya kukabidhi zawadi amezungumza na kusema kuwa washindi wote wamejikita katika haki za binadamu kuanzia za wanawake, wahamiaji, na a zaidi ya yote..

Sauti
3'12"
PICHA:IOM/Muse Mohammed

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa Uhamiaji.

Uhamiaji ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi, nguvu na ufahamu. Uhamaji unawaruhusu watu kutafuta fursa mpya, kunufaisha jamii wanakotoka na wanakohamia pia.

Lakini uhamiaji unaporatibiwa vibaya, unaweza kuchochea mgawanyiko katika jamii, kuwaweka watu katika unyonyaji na unyanyasaji na kupunguza imani kwa serikali.

Mwezi huu, dunia ilipiga hatua kwa kuidhinisha mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama, uliopangwa vizuri na wa kawaida. 

Sauti
1'23"
Picha: RET Liban

Changamoto za maisha zilinisukuma kuwa mchechemuzi- Rebeca Gyumi mshindi wa tuzo ya haki za binadamu 2018!

Mshindi wa tuzo ya mwaka huu haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Rebeca Gyumi kutoka Tanzania ambaye hii leo anakabidhiwa tuzo hiyo amezungumzia kile kilichomsukuma kuwa mchechemuzi wa  haki hususan za watoto wa kike kwenye taifa lake hilo la Afrika Mashariki.

Rebecca ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya ‘Msichana Initiative’ nchini Tanzania kwa miaka 8 amekuwa akihoji uhalali wa ibara ya 13 na 17 ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 nchini humo ambayo inahurusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 na 15 kwa ridhaa ya wazazi au mahakama.

Sauti
2'43"

11.12.2018

Leo ni siku ya milima duniani. Umoja wa Mataifa unapigia chepuo maeneo hayo kwa kaulimbinu milima ni muhimu. Biashara mtandaoni ikiwezeshwa yaweza kuliinua bara la Afrika  yasema UNCTAD, Mradi wa Benki ya Dunia Niger wakomesha hamahama ya wananchi kutokana na ukame.

Sauti
12'19"
UN Picha/Greg Kinch

Katu mtu au taasisi au serikali isijinasibu kuwa haki fulani ni za mtu au kundi fulani

Leo tarehe 10 Desemba mwaka 2018 ni kilele cha maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani ambapo katika mfululizo wa wetu wa kuchambua ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu, tunatamatisha kwa kuangazia ibara ya 30. Ibara hii inaeleza baya kuwa haki zote zilizomo kwenye tamko hilo lililopitishwa tarehe 10 Desemba mwaka 1948 huko Paris, Ufaransa haziachanishiki. Je hii ina maana gani, wakili Jebra Kambole, kutoka Tanzania ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu anafafanua.

 

Sauti
1'35"