Ukosefu wa elimu watumbukiza wengi kwenye ajira zisizo rasmi- Ripoti
Watu bilioni 2 kote ulimwenguni wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi na idadi kubwa ni katika nchi zinazoendelea na zile zinazoibuka kiuchumi.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO iliyochapishwa hii leo ikijikita katika takwimu za wanawake na wanaume walio kwenye sekta hiyo.
Ripoti inasema idadi hiyo ni zaidi ya asilimia 61 ya watu wote walioajiriwa duniani ikitanabaisha kuwa kiwango kidogo cha elimu ni kichocheo cha watu kuingia kwenye sekta hiyo.