Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

OCHA/Giles Clarke

UN na fursa ya kuleta nuru Hodeidah

Matukio kwenye uwanja wa vita ni kikwazo kwenye mchakato wa amani nchini Yemen, lakini mazungumzo ya kisiasa ni kipaumbele cha juu cha kutatua mgogoro huo, amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen katima mahojiano maalum na Idhaa ya  Umoja wa Mataifa.

Bwana Griffiths amesema kuwa kipaumbele kikuu na cha juu ni kuwezesha mazungumzo ili kukomesha vita akisema kuwa “Hodeida ni suala la kipekee na muhimu, lakini si muhimu zaidi kuliko suala la suluhisho la kisiasa." 

Sauti
3'2"

Uyatima hauhusiani kamwe na kipaji cha mtoto.

Watoto yatima au wanaoishi katika mazingira ya umasikini nchini Tanzania  mara nyingi hukosa fursa za maendeleo kielimu hata  kimaisha kwa sababu ya kutokuwa na ujuzi wowote limesema shirika lisilo la kiserikali la COMPASSION ambalo ni la kidini  linalowasaidia watoto na vijana yatima katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s.

Sauti
2'15"
UN/ Hubertus Juergenliemk

Tusisubiri kukabili ugaidi badala yake tuuzuie- Guterres

Masuala la wapiganaji mamluki, ushawishi wa vijana kutumbukia kwenye vitendo vya kigaidi na kitendo cha vijana hao kuona wameenguliwa kwenye masuala yanayowahusu yameangaziwa katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kukabiliana na uagidi ulioanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

 

Sauti
3'20"
UNHCR/Colin Delfosse

Kuwa mlemavu sio kulemaa: Dr. Sankok

Bado katika jamii nyingi duniani watu wenye ulemavu wanapitia changamoto kubwa ikiwemo kutengwa na kunyanyapaliwa na jamii lakini wengine hata na familia zao. Elimu ya ziada inatakiwa kuhakikisha jamii inaelewa kwamba kuwa na ulemavu wa viungo sio kulemaa akili na pia mchango wa watu wenye ulemavu ni mkubwa kwa jamii na unapaswa kuthaminiwa.

Sauti
1'50"
UNHCR/Ivor Prickett

Vita dhidi ya ugaidi yashika kasi mashinani

Kila uchao, magaidi wa kitaifa na kimataifa wanaibuka na mbinu mpya, vivyo hivyo tunapaswa kusaka mbinu mpya za kukabili vitendo hivyo viovu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akifungua kikao cha ngazi ya juu chenye lengo la kukabili ugaidi duniani.

Sauti
1'56"

Mbadala wa Oxytocin kuokoa wanawake wengi nchi zenye joto kali

Tatizo la wanawake kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua linaonekana kupata tiba mujarabu baada ya wataalamu kubaini dawa mpya isiyohitaji kuhifadhiwa kwenye jokofu kama ilivyo kwa dawa ya sasa iitwayo Oxytocin.

Dawa hiyo mbadala,  Carbetocin inafuatia utafiti uliofanywa na shirika la afya duniani, WHO na mshirika wake MSD, na majaribio ya dawa hiyo kufanyika katika nchi 10 duniani.

Sauti
1'51"