Mafuriko Kenya: UNICEF yapatia wakazi wa Kaunti ya Mto Tana fedha za kujikimu
Mvua za El-nino zikiendelea kutikisa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo taifa la Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza limepatia msaada wa hali na mali wakazi wa kaunti ya mto Tana walioathiriwa na mafuriko hayo.