Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mgonjwa anayeugua kipindupindu akitibiwa Tukombo kaskazini mwa Malawi. (Maktaba)
© UNICEF

Mkutano wa dunia kuhusu afya wakubaliana kuhusu marekebisho ya Kanuni za Afya za Kimataifa

Katika hatua ya kihistoria, Mkutano wa 77 wa Dunia kuhusu Afya (WHA77), ambao ni mkutano wa kila mwaka wa nchi wanachama 194 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, leo umekubali fungu la marekebisho muhimu ya Kanuni za Afya za Kimataifa (2005) (IHR) na kutoa ahadi madhubuti za kukamilisha ndani yam waka mmoja mazungumzo kuhusu makubaliano juu ya janga la afya la kimataifa ndani ya mwaka, ikiwezekana mapema iwezekavyo.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yana wasiwasi mpya kuhusu athari za uvutaji sigara kwa vijana.
© Unsplash/Tobias Tullius

Chonde chonde walindeni vijana dhidi ya mbinu za biashara ya tumbaku: WHO

Katika siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na kampuni ya kimataifa ta STOP inayofuatilia masuala ya tumbaku wamezindua wamezindua ripoti "Kuunganisha kizazi kijacho," ripoti inayoangazia jinsi tasnia ya tumbaku na nikotini husanifu bidhaa, kutekeleza kampeni za uuzaji na kufanya kazi kuunda mazingira ya sera ili kuwachagiza vijana wa ulimwengu kuwa waraibu.

Mwanamume amebeba kifurushi cha biskuti ambazo zimeingia hivi karibuni kupitia baharini.
© WFP/Jaber Badwan

Misaada ya kibinadamu Gaza haitoshi kabisa: UN

Wakati jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi yake ya anga na mashambulizi ya ardhini huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, wakazi wa eneo la Palestina linalokaliwa wanapokea msaada kidogo sana kiasi kwamba watoto zaidi na zaidi wanakufa kwa njaa, yameonya leo mshirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.