WHO yatoa orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa.