Tanzania inashikamana na ulimwengu kusongesha ajenda ya mazingira: Waziri Jafo
Mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo umekunja jamvi jijini Nairobi Kenya baada ya kukutanisha wadau zaidi ya 7000, kutoka nnyanja mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na changamoto kubwa tatu zinazoikabili dunia ambazo ni mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayoanuai na uchafuzi wa mazingira. Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano.