Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tukipewa nafasi tuna mchango wa kulinda mazingira: UNEA6

Vijana tukipewa nafasi tuna mchango wa kulinda mazingira: UNEA6

Pakua

Wakati jijini Nairobi Kenya mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 ukielekea ukingoni leo ikiwa ni siku yake ya 4, vijana wanaoshiriki mkutano huo wamepaza sauti zai na kusistiza kuwa wakipewa nafasi basi wana mchango mkubwa katika vita dhidi ya uharibifu wa mazingira na kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDGs.  Leo mkutanoni huko Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS amezungumza na vijana wawili wanaoshiriki mkutano huo ambao ni wanaharakati wa mazingira wanaotumia sayansi na sanaa kuleta mabadiliko katika jamii na pia ndio waliobuni sanaa ya jukwaa la mbao ambalo limewekwa kwenye lango la UNEA6 likipewa jina “Get your Seat at the Table”

Audio Credit
Evarist Mapesa/Stella Vuzo
Sauti
3'49"
Photo Credit
Stella Vuzo/UNIS Nairobi