Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/John Kabambala

Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine na FAO Tanzania wapima udongo katika wilaya 6 Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo.

Sauti
5'59"
© FAO/Alisa Suwanrumpha

Mradi wa FAO wa kupunguza upotevu wa chakula wazaa matunda nchini Thailand

Kupunguza upotevu wa chakula na taka kuna jukumu muhimu katika kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula.

Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs inataka kupunguza nusu ya upotevu wa chakula duniani kwa kila mtu katika viwango vya rejareja na walaji wa mwisho na pia inapigia chepuo kuimarisha minyororo ya uzalishaji na usambazaji wa chakula.

Sauti
3'19"
UN News/Evarist Mapesa

Kliniki tembezi nchini Tanzania yasaidia kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu

Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani, wakuu wa nchi na serikali wamekutana katika mkutano wa pili wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa  kutathmini mwelekeo wa Kifua Kikuu au TB kufuatia azimio la kisiasa la mwaka 2018 ambalo pamoja na mambo mengine linalenga kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.  

Audio Duration
5'38"
UNICEF Kenya

UNICEF: Apu ya OKY na hedhi salama yasongesha SDG 3

Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limezindua apu maalum ya wasichana kufuatilia maelezo wakati wa hedhi. Apu hiyo ni mahsusi kwa wasichana wa mataifa yanayoinukia na yaliyo masikini. Apu hii inaleta matumaini wakati huu ambapo viongozi wa dunia wanakutana New York, Marekani kutathmini maendeleo ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Thelma Mwadzaya amefuatilia na kutuletea makala kuhusu apu hiyo, iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. 

 

Sauti
2'47"
UN News/Flora Nducha

Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania

Wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa hapa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu wiki ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , tunaelekea Tanzania ambako katika pitapita zake, Flora Nducha alipokuwa jijini Dar es Salaama alikutana na mmoja wa vijana wajasiriamali kwenye kisiwa cha Bongoyo waliokumbatia wito wa kupambana na jinamizi la mabadiliko ya tabianchi, akamweleza  Flora kuwa mbali ya kujipatia kipato kutokana na utalii endelevu ana jukumu kubwa pamoja na baadhi ya vijana wenzie la kul

Sauti
4'26"
John Kabambala

Mradi wa stadi za maisha waleta manufaa kwa wanafunzi wa kike Tanzania

Shirika la Campaign for Female Education au CAMFED kwa kushirikiana na wizara za Elimu Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania wanatekeleza mradi wakutoa elimu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike katika shule za sekondari za serikali lengo likiwa ni kuboresha stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike na kuwapa fursa zaidi za elimu na ujifunzaji.

Sauti
4'52"
UNCDF Tanzania

Mradi wa UNCDF Tanzania wawezesha kaya kuondakana na nishati hatarishi ya kupikia

Nchini Tanzania kuna kaya nyingi ambazo zinatumia mkaa, kuni na mafuta ya taa kama tegemeo kuu la mapishi ya nyumbani, nishati ambazo si rafiki sio tu kwa mazingira bali pia afya ya mamilioni ya binadamu. Lakini sasa kuna mabadiliko,wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo nishati jadidifu na salama; wakati huu ambapo pia wakuu wa nchi watakutana jijini New York, Marekani kutathmini hatua zipi zimechukuliwa kubadili mwelekeo wa mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
4'38"
UNIS Nairobi

Amini Sayansi na sikilizeni sauti za watoto na vijana - Vijana katika mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi

Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi uliokunja chamvi hii leo jijini Nairobi nchini Kenya, umeleta pamoja vijana wanaharakati wa tabianchi kutoka nchi zote barani Afrika.  Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS Nairobi amekutana na baadhi ya vijana hao kandoni mwa mkutano huo na wanaeleza mawazo yao na walichojifunza.

Sauti
4'19"
© UNICEF/Gwenn Dubourthoumieu

Ndoto za kuwa daktari au Mwalimu Mkuu kwa watoto hawa zitatimia?

Ijapokuwa ni wakimbizi wa ndani na wanaishi kwenye kituo cha kuhifadhi wakimbizi wa ndani cha Bushagara, mjini Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mtoto Irene anataka kuwa daktari, na Christelle anataka kuwa Mwalimu Mkuu. Ingawa hivyo, elimu bado ni changamoto kubwa kwa watoto milioni 2.4 wakimbizi wa ndani nchini DRC hususan majimbo ya Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini ambao wanahitaji elimu kwa haraka. Hoja ni iwapo ndoto zao hizo zitatimia au ndio zitapeperushwa na vita inayoendelea nchini mwao na kuwafurusha kila uchao?

Sauti
3'32"