Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania

Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania

Pakua

Wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa hapa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu wiki ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , tunaelekea Tanzania ambako katika pitapita zake, Flora Nducha alipokuwa jijini Dar es Salaama alikutana na mmoja wa vijana wajasiriamali kwenye kisiwa cha Bongoyo waliokumbatia wito wa kupambana na jinamizi la mabadiliko ya tabianchi, akamweleza  Flora kuwa mbali ya kujipatia kipato kutokana na utalii endelevu ana jukumu kubwa pamoja na baadhi ya vijana wenzie la kulinda msitu wa Bongoyo na matumbawe ya Kisiwa hicho kilicho katika Bahari ya Hindi. Tusikilize mahojiano na kijana huyo anayeanza kwa kujitambulisha.

Audio Credit
Anold Kayanda/Flora Nducha
Sauti
4'26"
Photo Credit
UN News/Flora Nducha