Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/Frank Dejongh

Wanafunzi wenye ualbino tuna mahitaji mengi ili kuboresha taaluma yetu

Kama ilivyo nia ya jumla ya Malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa yaani SDGs kuwa asiwepo hata mmoja atakayeachwa nyuma katika kufikia maisha bora duniani, wanafunzi wenye ualbino katika shule ya msingi Mazinyungu iliyopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro Tanzania, wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia mahitaji muhimu kama vile mafuta ya kupaka, nguo za kufunika sehemu kubwa ya mwili wao, Kofia na miwani ili kuongeza ufaulu mzuri hasa kwa wenye uoni hafifu.

Sauti
3'22"
UN

Tanzania tunaenda vizuri katika sekta ya ukunga na uuguzi, ninachoomba ni kuongeza idadi ya wauguzi na wakunga- Beatrice Bernard Kambuga

Tukiendelea na mfululizo wa makala kuhusu wauguzi na wakunga, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha mwaka huu ulioteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa mwaka wa wauguzi na wakunga, leo tuko katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambayo kwa siku hupokea na kutoa huduma ya uzazi kwa wastani wanawake 8 hadi 10. Kupitia makala hii iliyoandaliwa na Nicolaus Ngaiza wa redio washirika Kasibante FM, Afisa muuguzi Mkunga mbobezi Beatrice Bernard Kambuga anaeleza chungu tamu za uuguzi na ukunga.

Sauti
5'47"
Photo: WHO/A. Esiebo

Hivi sasa Zanzibar tumefikia hadi asilimia 65 wanaojifungulia hospitalini, tunataka hata tufike asilimia 90 na zaidi- Azzah Amin Nofli

Miaka ya nyuma watu wengi visiwani Zanzibar walikuwa wanaamua kujifungulia zaidi nyumbani kuliko kwenda Hospitali. Miongoni mwa sababu zilikuwa ni umbali pamoja na uhaba wa miundombinu; hiyo ni kwa mujibu wa Bi Azza Amin Nofli, Afisa programu wa afya ya uzazi, wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia idadi ya watu, ofisi ndogo ya Zanzibar. Lakini hivi sasa idadi ya wanaotaka kujifungua wakiwa katika mikono ya wataalamu hospitalini imeongezeka kiasi cha kufikia asilimia 65.

Sauti
4'3"
UNFPA Mozambique

Wakunga na wauguzi wana mchango mkubwa katika afya ya mama na mtoto-Bi.Mafuru

Mwaka 2020 ni “Mwaka wa wauguzi na wakunga” ambapo shirika la afya ulimwenguni limesema dunia itahitaji ongezeko la wauguzi na wakunga milioni 9 ili kutimiza ahadi ya kutoa fursa ya huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Wakati wanataaluma hawa ambao wanakuwa na mchango mkubwa kiafya katika jamii wakienziwa, umuhimu wao bado ni mkubwa kwani wanategemewa kwa kiasi kikubwa.

Sauti
5'25"
National Institute of Allergy and Infectious Diseases, NIH, US

Kenya kuhakikisha kuna miakakati endapo Virusi vya Corona vitazuka:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO jana Alhamisi limetangaza kuwa virusi vipya vya corona ni dharura ya afya ya kimataifa inayotia wasiwasi likizitaka nchi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa endapo virusi hivyo vitazuka katika nchi zao. Kwa sasa virusi hivyo kitovu chake kimekuwa mji wa Wuhan nchini China ambako Kwa mujibu wa WHO jumla ya visa 9692 vimethibitishwa katika majimbo 31, na kati ya hivyo watu 1239 wako katika hali mbaya, 213 wamefariki dunia na wagonjwa 103 wametibiwa, kupona na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Na nje ya China kuna visa 68 vilivyothibitishwa katika nchi 18.

Sauti
5'41"
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch

Kumbukumbu na mikakati ya kupambana na nzige, Uganda

Wakati shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeonya juu ya janga la njaa katika ukanda wa Africa Mashariki  na pembe ya Afrika kutokana na uvamizi wa nzige nchini Ethiopia, Somalia na Kenya. Nchini Uganda hofu inazidi kutanda wakati ambapo nzige hao waperipotiwa kuvamia maeneo ya mpaka wake na Kenya, na kuharibu mazao ya kilimo na mimea katika mamilioni ya ekari. FAO imeitahadharisha Uganda na Sudan Kusini kuwa makini na kuchukua hatua ili kukabiliana na wimbi hilo la nzige endapo litazuka.

Sauti
3'48"
© UNICEF/Naftalin

Tunawaondoa wasichana wanaojiuza katika shughuli hiyo na kuwafundisha ujasiriamali- Carol Evelyn Nzogere

Moja ya azma ya jumla ya kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu yaani SDGs ni kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma bila kujali hali yake katika jamii. Shirika lisilo la kiserikali la Christ’s Daughters mjini Mwanza Tanzania chini ya Uongozi wa Carol Evelyn Nzogere wanawatafuta na kuwashawishi wasichana wadogo wanaojihusisha na biashara ya ukahaba ili kuwabadilisha na kuwaelimisha kuhusu ujasiriamali kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuokoa afya zao.

Sauti
4'11"
UN News/Patrick Newman

Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wanawake na wasichana wanaonekana kidijitali-Sambuli

Kwa miaka mingi, wanawake walikuwa wakiachwa nyuma katika maendeleo na hata maswala ya kijamii ikichochewa na utamaduni na mitazamo dume kwenye jamii. Kwa kutambua hilo Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu linalenga kuziba pengo hilo ambalo kwa miaka limebinya haki za wanawake na wasichana. Moja ya maeneo ambako mwanamke ameachwa nyuma ni ulimwengu wa dijitali na kwa kutambua hilo Katibu Mkuu aliunda jopo maalum kwa ajili ya kusongesha malengo hayo mbele.

Sauti
3'39"
UN Environment/Hannah McNeish

Mabadiliko ya tabianchi yametuathiri sana watoa tiba za asili- Mugisha John

Wakati tukiwa tumeingia katika muongo wa ukamilishaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, dunia inahaha kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaiweka sayari dunia katika hatari ya kukumbwa na majanga mbalimbali. Uharibifu wa mazingira si tu unaathiri moja kwa moja hali ya hewa kama vile ukame, upepo mkali na majanga mengine, pia kupitia makala hii iliyoandaliwa na Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe FM ya mkoani Kagera, mtaalamu wa tiba asilia Mugisha John wa Kayanga Karagwe anaeleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri kazi yao ya utafutaji wa tiba za mitishamba.

Sauti
3'26"
World Bank / Sarah Farhat

Tanzania imepiga hatua katika kuhakikisha kila mtoto anaandikishwa shuleni japo changamoto zipo

Stella Vuzo wa UNIC Dar es Salaam anamuhoji Ayubu Kafyulilo mtaalamu katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anayesimamia masuala ya ujifunzaji na elimu kwa ajili ya vijana na watoto ambao wako katika mazingira magumu na walio nje ya shule. Kwanza anaanza kwa kueleza hali ya elimu ikoje nchini humo baada ya kuanza kwa mfumo wa elimu bila malipo kwa ngazi ya kuanzia elimu ya awali, msingi hadi kidato cha nne.

Audio Duration
6'37"