Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

World Bank/Maria Fleischmann

COVID-19 yazidisha changamoto za chakula Uganda

 Njanga la virusi vya corona au COVID-19 limewaacha raia wengi nchini Uganda wakiwa na changamoto ya kipato  hali ambayo

imechangia kuongeza changamoto ya uhakika wa chakula.  Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego  mevinjari katika maeneo

mbalimbali kuangazia changamotot za upatikanaji wa achakula na lishe wakati huu ambapo mamilioni ya wanannchi wa kipato

cha chini wanakabiliwa na hatua za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kwa kutokwenda kazini, kufanya biashara   na hata

Sauti
4'3"
UNICEF/UNI212592/Tremeau

Digrii zangu mbili nimeziingiza katika uuzaji makande na ninafaidika sana- Nancy Lema

 Tatizo la ajira kwa vijana nchini Tanzania limeendelea kuwa changamoto kwa vijana wengi, baadhi  uhitimu elimu ya juu na vyuo vya kati huku wakiingia mtaani na kuisaka ajira kwa muda mrefu bila mafanikio. Kwa mujibu wa ripoti ya juu ya takwimu za utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi uliofanywa na Shirika la Takwimu nchini Tanzania (NBS) mwaka 2014, kuwa  watu elfu 23, sawa na asilimia 10 ya nguvu kazi, hawana kazi.

Sauti
4'2"
UN News/Assumpta Massoi

Wananchi wanaelewa kuhusu mabadiliko ya tabianchi baada ya kuiona hali halisi

 Mafuriko, mvua za kupindukia, ukame na kuyeyuka kwa barafu ni ishara kubwa ya mabadiliko ya tabianchi lakini ni hadi wakazi wa ulimwengu wayashuhudie ndipo wanaamini, hivyo ndivyo anavyoeleza Kaimu Afisa Mazingira wa wilaya ya Pangani katika mahojiano na Saa Zumo wa Redio washirika Pangani FM, kuhusu hatua na harakati zinazofanywa na mamlaka ya wilaya ya Pangani katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
2'19"
© UNICEF/Frank Dejongh

Unyanyapaa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya COVID-19 Uganda

Suala la unyanyapaa wa aina yoyote ile ni mtihani mkubwa katika jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao hutoa wito kila uchao kuhakikisha changamoto hiyo inatokomezwa .Wakati huu wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 unyanyapaa umeelezwa kujitokeza na kusababisha changamoto kwa wagonjwa na washukiwa na hata kuwafanya wengine kutojitokeza kufanya vipimo hali ambayo shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kuwa ni hatari kubwa na kikwazo cha kupambana na ugonjwa huo.

Sauti
6'25"
UNFPA/Ollivier Girard

Baada ya mimba ya utotoni , nina matumaini ya Maisha:Msichana Lydia

Mimba za utotoni ni changamoto kubwa na tishio kwa mustakbali wa wasichana wengi ambao hulazimika kuacha shule na kuwa mama katika umri mdogo na wengine hata kujikuta katika ndoa za utotoni.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa vyote viwili mimba na ndoa za utotoni vinaweka hatarini Maisha ya wasichana hao na hasa pale wanapojaribu kutoa mimba kwa njia zisizo salama kwa kuhofia wazazi , majukumu na pia kuchekwa katika jamii.

Sauti
3'21"
World Bank/Curt Carnemark

Mvua za kiholela zinatuchanganya- wakulima

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ni mabadiliko ya tabianchi. Suala hili limezua sintofahamu miongoni mwa wakazi wa dunia hii kutokana na mabadiliko ya misimu ya mvua, jua na hata kupata vipindi vya mvua kupita kiasi. Wakulima wamechanganyikiwa bila kufahamu la kufanya. Miongoni mwao ni wakulima kutoka Boza wilaya ya Pangani mkoani Tanga nchini Tanzania. Uelewa wake kuhusu mabadiliko ya tabianchi uko vipi? Ungana basi na Saa Zumo wa radio washirika Pangani FM kutoka Tanzania.

Sauti
3'51"
Benki ya Dunia/Stephan Gladieu

Kazi ya bodaboda imeboresha maisha yangu na mume wangu-Cecilia Paul

Pamoja dunia hivi sasa kuwa na changamoto mpya kama mlipuko wa ugonjwa COVID-19, lakini mipango ya muda mrefu inaendelea kutekelezwa ili kutimiza kusudio kuu la kuyatimiza kwa ukamilifu malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030. Malengo yote kwa ujumla wake yanakusudia kuifanya dunia kuwa mahali bora pa kuishi na ili kufikia hapo ni jukumu la kila mtu kushiriki harakati hizi.

Sauti
3'45"
© UN-Habitat/Kirsten Milhahn

Vijana Mwanza Tanzania wabuni mashine ya kusambaza maji kiteknolojia

Vijana jijini Mwanza Tanzania wamebuni mradi wa maji safi na salama kwa kutengeneza mashine za kielekroniki ikiwa ni sehemu ya juhudi zao kutimiza lengo namba sita la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDG ambayo yanategemewa kuwa yamekamilishwa kikamilifu ifikapo mwaka 2030. Lengo namba 6 la SDGs linazungumzia upatikanaji wa maji safi na salama na kujisafi. Vijana hao wahitimu wa Chuo Kikuu wameupa jina la ECO WATER mradi wao huo na mtumiaji hutumia kadi maalumu ya kielektroniki ili kupata huduma ya maji.

Sauti
4'2"
UNICEF/UN0156352/Dubourthoumieu

Zamani tulipeleka watoto kliniki muda tuliopenda lakini mafunzo ya TAMWA yametufungua- Mwanzo Mgumu

Afya ya mama na mtoto ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na nguvu kazi bora. Afya hii huanzia tangu hata kabla ya ujauzito hadi ujauzito wenyewe, kujifungua na hata baada ya kujifungua. Umoja wa Mataifa unatambua changamoto walizo nazo wanawake hususan maeneo  ya mashinani katika kupata huduma bora za afya ya uzazi ikiwemo lishe bora kwa mjamzito na pia kwenda kliniki ili kufahamu maendeleo ya mtoto aliye tumboni.

Audio Duration
4'52"