Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunawaondoa wasichana wanaojiuza katika shughuli hiyo na kuwafundisha ujasiriamali- Carol Evelyn Nzogere

Tunawaondoa wasichana wanaojiuza katika shughuli hiyo na kuwafundisha ujasiriamali- Carol Evelyn Nzogere

Pakua

Moja ya azma ya jumla ya kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu yaani SDGs ni kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma bila kujali hali yake katika jamii. Shirika lisilo la kiserikali la Christ’s Daughters mjini Mwanza Tanzania chini ya Uongozi wa Carol Evelyn Nzogere wanawatafuta na kuwashawishi wasichana wadogo wanaojihusisha na biashara ya ukahaba ili kuwabadilisha na kuwaelimisha kuhusu ujasiriamali kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuokoa afya zao. Katika mahojiano haya yaaliyofanyika mjini New York Marekani, Bi Nzogere aanaeleza namna wanavyofanya shughuli zao akianza na walivyolipata jina la taasisi yao.

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'11"
Photo Credit
© UNICEF/Naftalin