Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN/Emma Zibiliza

Nilijifunza mtandaoni kutengeneza viungo vya chai kisha nikaboresha ujuzi SIDO- Emma Zibiliza 

Emma Zibiliza ni kijana msomi nchini Tanzania ambaye amesukumwa na mambo mawili ya msingi kuingia katika ujasiriamali. Kwanza ni kupambana na hali ya ukosefu wa ajira iliyoko duniani, ambapo kwa hili analenga kujikwamua, kuwakwamua vijana wenzake kwa kuwaajiri, na pia kuwapa kipato wakulima wa malighafi anazozitumia katika mradi wake mpya wa kusindika mazao ili kutengeneza viungo vya chai.

Sauti
4'3"
OCHA/Steve Hafez

Mkimbizi nchini Uganda aeleza alivyopata moyo wa kulea mtoto aliyekimbia bila wazazi.

Kutokana na mizozo ya bunduki maelfu ya watoto hulazimika kukimbia nchini mwao bila kusindikizwa na wazazi au mtu mzima yeyote na kujikuta katika nchi jirani. Mara nyingine hujikuta mikononi mwa wanaowafanyia ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo ukatili wa kingono kwa watoto wa kike chini ya mwavuli wa kuwalea. Kulingana na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ya mwezi Machi mwaka huu 2020, Uganda ilikuwa na watoto elfu arubaini na mmoja na arubaini na mmoja 41,041 waliokimbia bila wazazi au kutenganishwa na familia zao.
Sauti
4'2"
UN/ John Kibego

Hata kama corona imetuingilia, bado tunaamini bado maisha yako mbele-Wanafunzi wakimbizi Uganda

Makala ifuatayo inamulika changamoto wanazokumbana nazo wanafunzi wakimbizi ambao hivi sasa wanalazimika kusalia majumbani ndani ya kambi baada ya shule kufungwa nchini Uganda ili kukabiliana na COVID-19. Mwandishi wetu John Kibego anazungumuza na wanafunzi Feza Kabera na Shamil Bao Yahaya ambao wanaeleza jinsi gani wanavyohimili vishawishi vya kupata mimba za utotoni na kujiunga na vikundi vya watumiaji madawa ya kulevya miongoni mwa mengine wakati huu wakiwa majumbani katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali.

 

Sauti
3'37"
UN-Habitat/Nathan Kihara

Tunahifadhi mazingira huku tukijipatia kipato-Vijana Kibera, Kenya.

Kutokana na ukosefu wa ajira kwenye nchini  nyingi  ni kawaida watu kutafuta na kubuni njia za kukidhi mahitaji  yao ya kila siku. Mtaani Kibera mjini Nairobi, vijana wameanzisha kikundi ambacho hivi sasa  kinaendelea na mradi ya kukusanya taka na kuzitumia kuunda vifaa mbalimbali kisha kuviuza kupitia mradi ujulikanao kama 'Slum going green and clean', ikiwa pia ni njia ya kusafisha mazingira. Jason Nyakundi amezungumza na kiongozi wa kikundi hicho Brian Nyabut

Sauti
3'21"
UN/ John Kibego

Mustakbali wa wanafunzi wakimbizi wamulikwa kati ya changamoto ya COVID-19, Uganda

Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na nchi nyingi duniani kama sehemu ya njia za kudhibiti kuenea kwa COVID-19, zimeathiri vibaya Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs likiwemo lile namba nne linalochagiza fursa za elimu bora. Nchini Uganda, kufungwa kwa taasisi za elimu ni miongoni mwa hatua za kwanza kabisa kuchukuliwa na hatimaye kuathiri moja kwa moja wanafunzi zaidi ya milioni 15. Hata hivyo serikali imetumia mbinu mbalimbali ikiwemo kusambaza masomo kupitia matangazo ya redio na televisheni ambavyo havijaweza kuwafikia wote.

Sauti
3'57"
UN/Ahimidiwe Olotu

Bila mitandao ya kijamii ni changamoto zaidi kufikisha elimu kwa vijana hasa wa vijijini- Tanzania Youth Aviation Foundation

Uzoefu wa kawaida unaonesha kuwa moja ya kazi ambazo ni ndoto za watoto wengi wakati wa ukuaji wao ni urubani wa ndege. Kwa sababu mbalimbali, moja kuu ikiwa ni kukosekana kwa taarifa za kutosha kuhusu elimu ya usafiri wa anga, inawafanya  watoto wengi kuipoteza ndoto hiyo na kuingia katika tasnia nyingine.

Sauti
4'3"
UN/ John Kibego

Wanawake wachimba chumvi waomba msaada, walalamikia vikwazo vya kuzuia COVID-19, Uganda

Nchini Uganda,katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo kandoni mwa ziwa Albert, wanawake wa eneo hilo wanaoegemea biashara ya uchimbaji na uuzaji chumvi maarufu kwa jina la chumvi ya Kibiro ambayo pamoja na matumizi ya kawaida ya mapishi hutumika pia katika dawa za asili wamejikuta katika wakati mgumu kwani ufikiaji wa maeneo ya ziwani umekubwa na changamoto lukuki ambazo ni pamoja na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na serikali ili kudhibiti kuenea kwa COVID-19, pia mafuriko yaliyoziba mtandao wa barabara, kufungwa kwa masoko, kufurushwa baadhi ya wakazi wa Ziwa Albert kwenye mialo iliobaini

Sauti
4'
UN News

COVID-19 imeongeza chumvi katika kidonda changu cha athari za mabadiliko ya tabianchi-Jemima Hosea 

Kutokana na mwamko wa watu nchini Tanzania kuyapenda mazingira ya nyumba zao, Jemima Hosea wa jijini Dar es Salaam, aliona hiyo ni fursa ya yeye kujipatia kipato kwa kuotesha na kuuza maua ya aina mbalimbali. Katika kipindi ambacho biashara yake ilikuwa imeanza kushamiri ndipo likaibuka janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19. Janga hili likaongeza machungu katika changamoto aliyokuwa anapambana nayo mfanyabiashara huyu-changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa amemtembelea Jemima na kutuandalia makala hii. 

Sauti
2'49"
UN-Habitat/Kirsten Milhahn

Haki za watoto zilindwe ili kulifikia lengo namba 3 na 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu

Lengo namba 3 la Maendeleo Endelevu linalenga afya na ustawi bora kwa jamii wakati lengo namba 4 likilenga elimu bora. Malengo haya kwa namna nyingine yanasaidia kulifikia lengo namba 5 ambalo linasisitiza usawa wa kijinsia na hata kuweza kulifikia lengo namba 11 linalolenga kuwa na jamii endelevu ifikapo mwaka 2030. Wadau wa haki za watoto wanasema ili kufanikiwa na kupata matunda ya malengo haya na mengine, ni muhimu kujali haki za watoto ili kupata kizazi bora cha siku za usoni ingawa safari hiyo bado ni ndefu kwani katika jamii bado kuna vitendo vinavyowanyima watoto fursa hiyo.

Sauti
3'11"