Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake ndani ya UN: Mambo yote unayopaswa kufahamu kuhusu CSW68

Balozi Mathu Joyini, (wa pili kutoka kulia) akifunga rasmi mkutano wa CSW67, anayemfuatia mwenye koti la buluu ni Mkuu wa UN Women, Bi. Sima Bahous
UN Women/Ryan Brown
Balozi Mathu Joyini, (wa pili kutoka kulia) akifunga rasmi mkutano wa CSW67, anayemfuatia mwenye koti la buluu ni Mkuu wa UN Women, Bi. Sima Bahous

Wanawake ndani ya UN: Mambo yote unayopaswa kufahamu kuhusu CSW68

Wanawake

Kila mwaka ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake dunini (CSW) hukutana mwezi Machi kujadili namna ya kukabiliana na ukosefu wa usawa ulioenea, unyanyasaji na ubaguzi wa wanawake unaoendelea kuwakabili duniani kote.

Huu hapa ni mwongozo mfupi wa mambo matano katika tukio hili la hadhi ya juu la Umoja wa Mataifa.

1. Kusukuma hatua kuchukuliwa kwa miongo minane

Kazi ya Kamisheni hiyo ilianza mwaka wa 1946, siku chache baada ya mikutano ya uzinduzi ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kumsikia Mama wa Rais wa zamani wa Marekani Eleanor Roosevelt na sehemu ya ujumbe wa nchi hiyo, akisoma barua ya wazi iliyoelekezwa kwa "wanawake wa dunia".

Bi. Roosevelt alikuwa ametoa wito kwa “Serikali za dunia kuhimiza wanawake kila mahali kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa na kimataifa, na kwa wanawake wanaotambua fursa zao kujitokeza na kushiriki katika kazi ya amani na ujenzi upya walivyofanya wakati wa vita na upinzani”.

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) ilianzisha kamisheni ndogo mara moja. Wanachama wake sita - China, Denmark, Jamhuri ya Dominika, Ufaransa, India, Lebanon na Poland - walipewa jukumu la kutathmini "matatizo yanayohusiana na hali ya wanawake" ili kuishauri Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, mtangulizi wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa. 

Katika ripoti yake ya kwanza, "wajumbe walizingatia kwamba kazi ya kamisheni ndogo inapaswa kudumu hadi wanawake wafikie kiwango cha kuwa katika usawa na wanaume katika nyanja zote za kibinadamu".

Tangu mwanzo kulikuwa na wito wa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuweka kipaumbele kwenye haki za kisiasa, "kwani maendeleo madogo yasingeweza kupatikana bila wao", pamoja na mapendekezo ya maboresho katika nyanja za elimu ya kiraia, kijamii na kiuchumi, ambayo "matatizo yanapaswa kushughulikiwa kwa wakati mmoja", ripoti ilisema. Aidha, ripoti ilitoa wito wa "Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake ili kuendeleza mpango".

Kufikia mwezi Juni 1946, ikawa rasmi Kamisheni ya Hali ya Wanawake, kama moja ya taaisi tanzu ya ECOSOC. Kuanzia 1947 hadi 1962, Kamisheni ilizingatia kuweka viwango na kuunda mikataba ya kimataifa ya kubadilisha sheria za kibaguzi na kukuza ufahamu wa kimataifa wa masuala ya wanawake.

Mkulima Biresaw, kutoka Ethiopia.
© World Bank/Dana Smillie
Mkulima Biresaw, kutoka Ethiopia.

2. Mikataba ya kihistoria ya kimataifa iliyopigwa

Kuanzia siku za awali za Kmaisheni, kitendo cha kuongezeka kwa wanachama wake kulichangia baadhi ya mikataba ya kimataifa iliyokubaliwa zaidi katika historia ya Umoja wa Mataifa. Hii hapa ni michache tu.

Ikimsaidia Bi. Roosevelt, mwenyekiti wa kamati ya kuandaa Tamko la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, Kamisheni ilifanikiwa kubishana dhidi ya marejeleo ya "wanaume" kama kisawe cha ubinadamu. Pia ilianzisha lugha mpya, iliyojumuisha zaidi katika toleo la mwisho la Mkutano Mkuu uliopitishwa mnamo 1948.

Mnamo mwaka 1963, juhudi za kujumuisha viwango vya haki za wanawake zilisababisha Baraza Kuu kuomba Kamisheni kuandaa Azimio la Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake, ambalo lilipitisha mnamo mwaka 1967.

CSW ilikuwa muhimu katika kupitishwa kwa Azimio la Beijing la 1995 na Mfumo wa Utekelezaji, waraka muhimu wa sera ya kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia.

Mwanamke kutoka akiuza mazao ya misitu katika soko la ndani.
UNDP India
Mwanamke kutoka akiuza mazao ya misitu katika soko la ndani.

3. Nchi nyingi, mahitaji zaidi

Kwa kuongezeka kwa wanachama wa Umoja wa Mataifa na ushahidi unaoongezeka katika miaka ya 1960 kwamba wanawake waliathiriwa kwa kiasi kikubwa na umaskini, CSW ilizingatia mahitaji ya wanawake katika maendeleo ya jamii na vijijini, kazi za kilimo, uzazi wa mpango, na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Pia ilihimiza mfumo wa Umoja wa Mataifa kupanua usaidizi wa kiufundi ili kuendeleza maendeleo ya wanawake, hasa katika nchi zinazoendelea.

Kazi ya hali ya juu katika suala hili ilifanyika, CSW pia ilitayarisha Mkataba unaofunga kisheria wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) mwaka 1979.

Katika muongo huo, Umoja wa Mataifa ulitangaza mwaka 1975 kuwa Mwaka wa Kimataifa wa Wanawake na kuitisha Kongamano la Kwanza la Dunia kuhusu Wanawake, lililofanyika Mexico. Mnamo mwaka 1977, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, iliyoadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka.

Mnamo mwaka wa 2010, baada ya mazungumzo ya miaka mingi, Baraza Kuu lilipitisha azimio la kuunganisha sehemu na idara zinazohusiana za Shirika kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN Women), ambalo linaendelea kushirikiana kwa karibu na Tume.

Mabadiliko ya tabianchi yamefanya maisha ya wakulima wanawake kuwa magumu zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Mwanamke akinyunyizia maji mboga katika bustani ya soko iliyoanzishwa kwenye ardhi iliyoharibiwa zamani huko Ouallam, Niger. Bustani hiyo inashirikiwa na wakimbizi, watu waliokimbia makazi yao na wenyeji.
© UNHCR/Colin Delfosse
Mwanamke akinyunyizia maji mboga katika bustani ya soko iliyoanzishwa kwenye ardhi iliyoharibiwa zamani huko Ouallam, Niger. Bustani hiyo inashirikiwa na wakimbizi, watu waliokimbia makazi yao na wenyeji.

4. Kushughulikia masuala yanayojitokeza

Vikao vya kila mwaka vinashughulikia na kutathmini masuala yanayojitokeza pamoja na maendeleo na mapungufu katika utekelezaji wa Jukwaa la Utendaji la Beijing. Nchi Wanachama kisha zinakubaliana juu ya hatua zaidi za kuharakisha maendeleo.

Tangu mwaka 2018, CSW imeshughulikia changamoto kama vile mabadiliko ya tabianchi, unyanyasaji wa kijinsia, na kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika kufanya maamuzi na katika mikakati ya maendeleo endelevu.

Ikipitisha programu za kazi za miaka mingi ili kutathmini maendeleo na kutoa mapendekezo zaidi ili kuharakisha utekelezaji wa Jukwaa la Utekelezaji, CSW inatuma mahitimisho yake yaliyokubaliwa kwa ECOSOC kwa hatua kuchukuliwa.

Kwa nia ya kuwafikia wanawake wote na kutomwacha mtu nyuma, Tume pia inachangia katika ufuatiliaji wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ili kuharakisha utekelezaji wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Mwanamke akitengeneza kompyuta ndogo kwenye duka lake la kutengeneza simu na kompyuta huko Taiz, Yemen.
© ILO/Ahmad Al-Basha/Gabreez
Mwanamke akitengeneza kompyuta ndogo kwenye duka lake la kutengeneza simu na kompyuta huko Taiz, Yemen.

5. Kufanyia kazi mazungumzo

Suluhu za kumaliza umaskini wa wanawake zinatambulika sana. Kuanzia kuwekeza katika sera na programu zinazoshughulikia ukosefu wa usawa wa kijinsia na kukuza wakala na uongozi wa wanawake hadi kuziba mapengo ya kijinsia katika ajira. Kufanya hivyo kungeinua zaidi ya wanawake na wasichana milioni 100 kutoka kwenye umaskini, kutengeneza nafasi za kazi milioni 300 na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 20 katika mabara yote.

Katika mwaka huu wa uchaguzi, watu bilioni 2.6 wanapopiga kura, wana uwezo wa kudai uwekezaji wa juu zaidi katika usawa wa kijinsia.

Masuala haya ya kubadilisha kabisa maisha, yanashughulikiwa katika kikao cha CSW cha mwaka huu wa 2024, ambapo wanachama wake 45 na maelfu ya washiriki kutoka kote ulimwenguni watazingatia mada "Kuharakisha mafanikio ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote kwa kushughulikia umaskini na kuimarisha taasisi na kufadhili kwa mtazamo wa kijinsia”.

Tume ya mwaka huu ya Hali ya Wanawake inafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kuanzia tarehe 11 hadi 22 Machi. 

Kupata maelezo zaidi kuhusu mkutano huu bofya hapa.

Ili kujifunza zaidi kuhusu vikao vya CSW vilivyopita na vya sasa, tembelea Historia Fupi ya Umoja wa Mataifa ya Tume ya Hali ya Wanawake.