Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mahojiano

Oscar Ikinya

Miaka 23 baada ya tukio la ugaidi Kenya bado athari zipo-Oscar Ikinya

Wakati dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya kumbukumbu na kuwaenzi waathirika wa ugaidi Agosti 21 Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kuendelea kushikamana na waathirika kwani Maisha yao yanabadilika kwa kiasi kikubwa kufuatia matukio waliyoyapitia, Hali ni kama hiyo kwa mgeni wetu wa leo manusura wa shambulio la kigaidi la Kenya la mwaka 1998. Amezungumza na Grace Kaneiya akiwa Nairobi Kenya kwa njia ya mtandao. Katika mazungumzo safari imeanzia miaka 23 iliyopita wakati wa tukio hadi sasa. Karibu.

Sauti
28'51"
UN News

Mahojiano la Mbunge Neema Lugangira wa Tanzania kuhusu nafasi ya mbunge kwa umma

Uwepo wa wabunge wenye nguvu ni msingi imara wa Demokrasia kwa mujibu wa lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa linalolenga amani, haki na taasisi thabiti. Hilo ni dhahiri kwa kuwa wawakilishi hao wa wananchi wanakuwa na uwezo wa kutunga sheria, kutenga fedha kwenda kufanya kazi ya utekelezaji wa sheria na sera walizozipitisha na kuwajibisha serikali iwapo haijatenda yale wananchi wanayakusudia kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii hususan walioko kwenye mazingira magumu. 

Kuelekea siku ya kimataifa ya Mabunge 30 Juni, Leah Mushi amefanya mahojiano na mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhusu nafasi ya wabunge katika kuhakikisha usalama wa wananchi wao hususani wakati huu dunia ikipambana na janga la corona au COVID19. kwanza anaanza kwa kujitambulisha 

Sauti
8'51"
UNIC/Stella Vuzo

Je wafahamu vinavyotibua bayonuai?

Muongo wa kurejesha bayonuai umezinduliwa rasmi mwezi huu wa Juni mwaka 2021 kwa lengo la kurekebisha kile ambacho mwanadamu amefanya kuharibu mazingira ya sayari dunia na vile vile kuchukua hatua kuepusha uharibifu. Je nini kinaharibu bayonuai? Lucy Igogo wa kituo cha habari cha  Umoja wa Mataifa UNIC jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini humo. Bi. Makenya anaanza kwa kuelezea chanzo cha muongo huo.

Sauti
10'37"
UN News/Siraj Kalyango

Msikate miti hovyo kwa kuwa jangwa lanyemelea

Ukataji holela wa miti kinyume na vibali ambavyo vinatolewa na serikali ni moja ya sababu za uharibifu wa mazingira nchini Kenya, amesema Isabella Masinde mtaalam wa mazingira, kutoka idara ya mazingira nchini humo.

Katika mahojiano  na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa  Mataifa mjini New York, Marekani, Bi.Masinde,Mkurugenzi wa Mazingira na ulinzi wa masuala ya  kijamii katika kamati ya kitaifa ya kupokea  malalamiko kuhusu mazingira nchini Kenya amesema.miongoni mwa mengine kuwa maendeleo yanaathiri mazingira   wakati ..mambo ya kufanya mipango ya matumizi ya hayo mazingira hayatekelezwi, lakini kama kungekuwa na utaratibu wa kujua kama kwa mfano miti ikitolewa miti elfu moja tutaendelea vizuri.