Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mahojiano

UN Video

Vijana tunachagiza mabadiliko ya kisera ili kulinda bahari - Nancy Iraba

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu bahari unaendelea huko Lisbon, Ureno. Mkutano huu umeanza tarehe 27 mwezi huu wa Juni na utamalizika tarehe 1 Julai 2022. Kabla ya kuanza kwa kikao cha ngazi ya juu, mkutano ulitanguliwa na jukwaa la vijana likileta pamoja wanaharakati na wachechemuzi vijana kuhusu masuala ya baharí wakionesha ubunifu wao wa jinsi ya kutatua dharura ya baharí, kama alivyooiita Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres .Miongoni mwa washiriki ni kijana Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dare es salaam nchini Tanzania. Hapa akihoijwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa anaelezea jukwaa linajikita na nini.

Sauti
1'32"
UN News Picha: Assumpta Massoi

Ujio wangu na ushiriki katika Jukwaa la watu wa asili umekuwa na matokeo chanya mashinani-Kiburo

Mkutano wa 21 wa Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, UNPFFII mwaka 2022 umefanyika kwenye makao makuu yake New York. Mkutano huo umewakutanisha watu wengi kutoka pembe zote za dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni Carson Kiburo kijana kutoka jamii ya watu wa asili ya Bondel la ufa kaunti ya Baringo nchini Kenya, amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii.

Sauti
9'13"
UN/ Anold Kayanda

UN haiwezi kusahau Pembe ya Afrika

Ukame unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi umesababisha watu takribani milioni 15 katika eneo la Pembe ya Afrika kukosa uhakika wa kupata chakula. Sasa Umoja wa Mataifa unafanya nini? Joyce Msuya, Msaidizi wa Katibu Mkuu na Naibu Mkuu wa OCHA anafafanua akianza kwa kueleza taswira ya njaa katika eneo hilo hususan Kenya, Ethiopia na Somalia.

Sauti
10'34"
Mahakama ya Kenya

Majaji wanawake Kenya tumeletea mabadiliko chanya - Jaji Okwengu

Tarehe 10 mwezi Machi mwaka 2022, kumefanyika maadhimisho ya kwanza ya siku ya majaji wanawake duniani. Siku hii imeadhimishwa na maudhui yakiwa "Haki katika Mtazamo wa Kijinsia." Lengo ni kuona ni kwa vipi majaji wanawake wanaweza kuwa chachu katika utoaji wa haki kwenye mahakama kwa kuzingatia kuwa tasnia hiyo imegubikwa na mfumo dume. Katika kufahamu ukweli wa hoja hiyo Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Jaji Hannah Okwengu wa Mahakama ya Rufaa nchini Kenya ambaye anaanza kwa kuelezea anajisikiaje kuwa Jaji kwenye tasnia iliyozoeleka kuwa ya wanaume wengi zaidi.

Sauti
15'14"
© UNICEF/Mulugeta Ayene

Ukame ukisogea wafugaji uzeni mifugo kuepusha hasara - Dkt. Mutungi

Huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika ambako huko kwa kipindi kirefu sasa njaa na ukame vimekuwa tatizo kubwa. Mwezi uliopita wa Januari shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO lilitoa ombi la zaidi ya dola milioni 138 za ufadhili wa dharura ili kusaidia watu milioni 1.5 walio hatarini katika jamii za vijijini huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. Kufahamu hali halisi mashinani iko vipi, Leah Mushi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Dokta. Paul Mutungi Afisa wa mashinani wa FAO akihusika na wafugaji katika Ukanda wa Afrika Mashariki na anaanza kwa kueleza hali ya kibinadamu ilivyo huko mashinani. 

Sauti
6'44"