Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano la Mbunge Neema Lugangira wa Tanzania kuhusu nafasi ya mbunge kwa umma

Mbunge wa Bunge la Tanzania Neema Lugangira.
UN News
Mbunge wa Bunge la Tanzania Neema Lugangira.

Mahojiano la Mbunge Neema Lugangira wa Tanzania kuhusu nafasi ya mbunge kwa umma

Masuala ya UM

Uwepo wa wabunge wenye nguvu ni msingi imara wa Demokrasia kwa mujibu wa lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa linalolenga amani, haki na taasisi thabiti. Hilo ni dhahiri kwa kuwa wawakilishi hao wa wananchi wanakuwa na uwezo wa kutunga sheria, kutenga fedha kwenda kufanya kazi ya utekelezaji wa sheria na sera walizozipitisha na kuwajibisha serikali iwapo haijatenda yale wananchi wanayakusudia kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii hususan walioko kwenye mazingira magumu. 

Kuelekea siku ya kimataifa ya Mabunge 30 Juni, Leah Mushi amefanya mahojiano na mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhusu nafasi ya wabunge katika kuhakikisha usalama wa wananchi wao hususani wakati huu dunia ikipambana na janga la corona au COVID19. kwanza anaanza kwa kujitambulisha