Mradi wa FAO wa uhimilishaji ng’ombe nchini Syria ni nuru katikati ya giza
Nchini Syria, miaka 10 ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe imeleta madhila ikiwemo watu kukimbia makwao lakini Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, FAO limewashika mikono wananchi ambao wanaendelea kushiriki shughuli za kilimo na ufugaji katika majimbo ya Aleppo, Al Hassakeh na Deir Ez-Zor.