La Ninã inatarajiwa baadaye mwaka huu lakini joto litasalia kuwa juu:WMO
Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO linatabiri kuongezeka kwa ukame katika baadhi ya maeneo duniani na kuongezeka kwa hatari ya mafuriko katika maeneo mengine.
Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO linatabiri kuongezeka kwa ukame katika baadhi ya maeneo duniani na kuongezeka kwa hatari ya mafuriko katika maeneo mengine.
Andrew Young, Balozi wa kwanza wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa mwenye asili ya Afrika akiwa anaandika historia hiyo amem mwagia sifa Ralph Bunche kuwa mtu aliyekuwa akimvutia
Wakati wa moja ya safari za mara kwa mara za Naomi Otua kumtembelea mjukuu wake James katika mji wa Assin Fosu kati kati mwa Ghana, aligundua kuwa kulikuwa na tatizo kubwa sana.
Nchini Cameroon, kijana mwanaharakati ambaye amegeuza maisha yake kutoka yale ya vurugu na ghasia hadi kuwe kijana mtetezi wa masuala ya raia na amani kwenye jamii yake amezungumza na Umoja wa Mataifa na kuelezea jinsi ambavyo anasaidia vijana wengine kukataa mizozo na badala yake wachukue dhima kubwa ya kujenga amani nchini mwao.
Muongo uliopita ulitajwa kuwa wenye viwango vya juu vya joto zaidi katika historia. Majanga yakiwemo moto wa nyika, mafuriko na vimbunga vinazidi kuongezeka huku viwango vya gesi chafuzi vikiwa ni asilimia 62 zaidi tangu wakati mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabianchi yalipoanza mwaka 1990.
'Tutafanya nini iwapo maji yataendelea kujaa?’ Hilo ni swali lililogubika kila mtu: Wamiliki wa nyumba, wakandarasi wa ujenzi, wajenzi, wakulima, wachuuzi sokoni, wanafunzi, wasafiri na bila shaka wafanyakazi wa maendeleo na kibinadamu.
Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ulitangazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kuwa janga la afya ya umma duniani tarehe 30 mwezi Januari mwaka 2020.
Pumla Ntalabati ni mfanyakazi mshauri wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Afrika Kusini, anasema janga la corona au COVID-19 limemfundisha za mengi, kuanzia amri ya watu kusalia majumbani hadi safari yam ilima na mabonde ya kuelimisha umma katika jimbo la Kwazulu Natal kwa kutumia usafiri wa lori la magurudumu 18.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameiasa dunia kutowasahau wajane hasa wakati huu wa janga la corona au COVID-19 ambapo wanaume wengi wanaendelea kupoteza maisha na kuwaacha wake zao wakihaha na familia.
Katika kufanikisha lengo la Muungano wa Afrika, AU kuhakikisha asilimia 60 ya wakazi wa bara lake wamepatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 ifikapo mwaka 2022, Benki ya Dunia na AU wametangaza ubia wa kuunga mkono mpango wa kikosi kazi cha Afrika cha kupata chanjo hizo, AVATT utakaoruhusu nchi za Afrika kununua na kusambaza dozi za chanjo kwa ajli ya watu milioni 400 barani kote.