Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Stadi za maisha ni muhimu hususani kwa vijana ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu

Stadi za maisha ni muhimu hususani kwa vijana ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu

Pakua

Nchini Tanzania Jumla ya Kaya 13,600 na vijana 2,700 wanatarajiwa kunufaika na tathmini ya upimaji stadi za maisha kwa kuangalia viwango vyao vya kujitambua, ushirikiano walionao kwao na kwa jamii, jinsi wanavyotatu matatizo pamoja na heshima binafsi jinsi wanavyojiheshimu wao, jamii na mali za wengine. Sifa zote hizo ni muhimu katika kusaidia wanajamii wa rika mbalimbali wanashiriki katika kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. 

Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation inatekeleza mradi huo ikilishirikisha Shirika la Uwezo Tanzania kusimamia upande wa Tanzania Bara ambapo mradi utafika katika katika Halmashauri za Wilaya 34, Hamad Rashidi ni mwanahabari kutoka Redio washirika wetu Tanzania Kidstime ya mkoani Morogoro amehudhuria mafunzo yaliyofanyika Mkoa wa Morogoro wakipewa wakufunzi watakaoenda kufundisha wapimaji wa tathmini ya stadi za maisha kwa vijana na kutuandalia makala ifuatayo. 

Audio Credit
Anold Kayanda/ Hamad Rashid
Audio Duration
4'8"
Photo Credit
UN News