Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya ujuzi yaliyofadhiliwa na ILO yamenikwamua kwenye biashara yangu ya chakula – Hamad Hamis

Mafunzo ya ujuzi yaliyofadhiliwa na ILO yamenikwamua kwenye biashara yangu ya chakula – Hamad Hamis

Pakua

Mwaka 2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 15 Julai kuwa Siku ya Stadi kwa Vijana Duniani, ili kusherehekea umuhimu wa kimkakati wa kuwapa vijana ujuzi wa kuajiriwa, kazi zenye staha na ujasiriamali. Tangu wakati huo, Siku ya Stadi kwa Vijana Duniani imetoa fursa ya kipekee ya mazungumzo kati ya vijana, taasisi za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET), makampuni, waajiri na mashirika ya wafanyakazi, watunga sera na washirika wa maendeleo.  

Mfano wa namna ujuzi kwa vijana unavyoweza kuleta tija katika maisha ya vijana na jamii kwa ujumla, ni kijana Ahmad Hamis wa Kigoma, kaskazinimaghariki mwa Tanzania, ambaye mafunzo aliyoyapata kwa ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO Tanzania, anasema maisha yake yanaenda vizuri mno kuliko awali. Mwandishi John Kabambala wa redio washirika Kidstime FM ya Morogoro, Tanzania, ameangazia maisha ya kijana huyo na kuandaa makala hii.  

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kabambala
Audio Duration
3'29"
Photo Credit
FAO Tanzania