Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikufahamu kuhusu zao la mwani, sasa limenibadilishia maisha yangu- Marinda

Sikufahamu kuhusu zao la mwani, sasa limenibadilishia maisha yangu- Marinda

Pakua

Wakati mkutano wa dunia kuhusu bahari umeanza leo huko Lisbon nchini ureno kujadili namna ya kuhakikisha bahari inalindwa ili jamii zinufaike na uchumi utokanao na shughuli za kwenye bahari au uchumi wa buluu sambamba na faida nyingine nyingi, tunaelekea kijiji cha Kibuyuni, eneo la Shimoni, kaunti ya Kwale nchini Kenya kusikia jinsi maisha ya wakulima wa zao la mwani linalolimwa baharini yalivyobadilika baada ya mradi wa shamba la mfano la mwani ulioanzishwa na Taasisi ya Utafiti wa Majini na Uvuvi ya Kenya KMFRI kuleta manufaa kwa wanakijiji zaidi ya 2500 wa kijiji hicho. Kabla ya mradi huo maisha ya wanakijiji hao yalikuwa duni na jengo pekee lililokuwa limeezekwa mabati lilikuwa ni msikiti, lakini sasa wananchi hawa wana uhakika wakupata dola 300 kila baada ya siku 45. Ni kwa vipi basi, tuungane na Leah Mushi katika makala hii iliyofanikishwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC nchini Kenya,

Audio Credit
Assumpta Massoi/Leah Mushi
Audio Duration
3'37"
Photo Credit
UN Video