Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu ana jukumu la kulinda mazingira ya bahari

Kila mtu ana jukumu la kulinda mazingira ya bahari

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani Umoja wa Mataifa unamchagiza kila mtu kuchukua hatua na kulinda mazingira ya bahari ambayo sio tu ni muajiri mkubwa wa sekta ya uvuvi duniani bali ni mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa duniani kote thamani ya soko la sekta ya bahari na rasilimali zake inakadiriwa kuwa ni dola trilioni 3 kwa mwaka au asilimia 5 ya pato la dunia ndio maana unaichagiza dunia kushikama kuchukua hatua kuilinda bahari kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho. Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya amekwenda Vanga Pwani ya Kenya katika bahari ya Hindi mpakani na Tanzania kuzungumza na wakazi wa eneo hilo je wanatambua umuhimu wa bahari? na nini wanafanya ili kuilinda, ungana naye katika makala hii.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Thelma Mwadzaya
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
© UNDP/Amunga Eshuchi