Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitandao ya kijamii inatusaidia lakini habari za uongo nazo ni changamoto - Kambini Lusenda, DRC

Mitandao ya kijamii inatusaidia lakini habari za uongo nazo ni changamoto - Kambini Lusenda, DRC

Pakua

Takribani miaka miwili iliyopita, Umoja wa Mataifa ulizindua mkakati wake na ukapewa jina "iliyothibitishwa" au “Verified initiative” ambao unataka watu kote duniani kutafakari kabla ya kusambaza taarifa au maaudhi kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ni moja ya njia inayotumiwa na jamii sio tu kwa mawasiliano kwa wapendwa wao bali pia kupata taarifa muhimu sehemu mbalimbali na za muhimu katika maisha ya kila siku. Katika Kambi ya Lusenda jimboni Kivu ya kusini mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakimbizi, hususani vijana wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kama vile Facebook na WhatsApp lakini wanasema kuwa moja ya changamoto ni kuwa wakati mwingine kunakuwa na habari za uongo zinazozagaa katika mitandao hiyo. Mwandishi wetu wa DRC, Byobe Malenga ametembelea kambi hyio na kuzungumza na baadhi ya vijana kuhusu suala hilo. 

 

Audio Credit
Leah Mushi/ Byobe Malenga
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
UPU