Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utimizaji wa SDGs unategemea juhudi za kutunza mazingira-WWF

Utimizaji wa SDGs unategemea juhudi za kutunza mazingira-WWF

Pakua

Utunzaji wa mazingira ni suala jumuishi kwani linaathiri kila mtu. Nchini Kenya wenyeji wa kaunti ya Naivasha, kufuatia mafunzo waliyopokeana shirika la World Wide Fund for nature (WFF) wanatunza mazingira na wakati huo huo kuimarisha kipato chao kwani kilimo kinategemewa kwa nafasi kubwa.

Kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi juhudi za serikali, mashirika binafsi na jamii zinahitajika ili kufanikisha lengo la malengo ya maendeleo endelevu SDGs na malengo yote kwa jumla.

Ili kupata undani wa mradi Grace Kaneiya amezungumza na Innocent Maloba kutoka shirika hilo la WWF,   linalofanya kazi katika takriban nchi 100 kote duniani ambaye anaanza kwa kuelezea kuhusu mradi wanaosimamia kaunti ya Naivasha nchini Kenya.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango/Grace Kaneiya/Innocent Maloba
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
Mradi wa kusaidia kuboresha mazingira kwa kulinda misitu na mito nchini Kenya.(Picha:UNEP)