Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu dawa za kulevya nchini Kenya
Wasomi wa kiislamu barani Afrika pamoja na wenzao kutoka bara Asia wamekamilisha mkutano wa siku nne mjini Mombasa, Kenya, kuzungumzia njia muafaka za kukabili utumiaji wa dawa za kulevya.Baadhi ya maafikiano katika mkutano huo ni kushirikisha jamii nzima katika kutatua tatizo la dawa za kulevya,
Nchi za pembe ya Afrika zaendelea kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula
Ripoti zimekuwa zikitolewa kuhusu hali kwenye pembe ya Afrika baada ya eneo hilo kukumbwa na ukame wa muda mrefu.
Dr wa Hospitali ya Panzi DR Congo ataka ushirikiano zaidi na UM
Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na kumuelezea nia ya ushirikiano baina ya hospitali yake, Umoja wa mataifa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini
Dr wa hospitali inayoungwa mkono na UM DR Congo apata tuzo
Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametunukiwa tuzo ya kiamataifa na ufalme wa Ubelgiji mwezi Mai mwaka huu kwa mchango wake katika jamii.
MKURABITA yaitwalia Tanzania tuzo ya UM ya utumishi wa umma
Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA umeisaidia Tanzania kujinyakulia tuzo ya utumishi wa umma Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Mataifa hasa kwa kuangalia ubunifu wa kuweza kuharakisha huduma nzuri kwa umma.
Waliowauwa walinda amani wa MONUSCO wahukumuwa DR Congo
Watu wanne miongoni mwa tisa wanaodaiwa kuwa waasi waliowawa askari watatu walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO miezi tisa iliyopita wamekatiwa hukumu na mahakama ya kijeshi nchini humo.
Katika vita vya ukimwi Tanzania kuongeza elimu, madawa na utafiti:Dr Bilal
Serikali ya Tanzania inasema pamoja na kupiga hatua katika vita dhidi ya ukiwmi bado ina safari ndefu ingawa zaidi ya asilimia 50 ya waathirika wanapata dawa za kurefusha maisha.
Ingawa bado ina changamoto Kenya inasema imepiga hatua katika vita vya ukimwi
Pamoja na kwamba mkutano wa ngazi ya kimataifa wa ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa umekamilika lakini vita dhidi ya ukimwi vinaendelea.
UM umezindua mpango kukabiliana na unyanyapaa kwa wenye HIV
Umoja wa Mataifa leo Juni 8 umezindua mpango maalumu wa kukabiliana na unyanyapaa kwa wafanyakazi wanaoishi na virusi vya HIV katika mada ya “unyanyapaa unachagiza maambukizi zaidi”.