Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa bado ina changamoto Kenya inasema imepiga hatua katika vita vya ukimwi

Ingawa bado ina changamoto Kenya inasema imepiga hatua katika vita vya ukimwi

Pakua

Pamoja na kwamba mkutano wa ngazi ya kimataifa wa ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa umekamilika lakini vita dhidi ya ukimwi vinaendelea.

Viongozina wawakilishi 3000 kutoka nchi zaidi ya 30 waliokuwa wakikutana wametoka na azimio la kuweka malengo ikiwa ni pamoja na kupunguza kwa asilimia 50 HIV ifikapo 2015, pia wanadhamiria kupunguza kwa nusu maambukizi ya HIV kwa wanaotumia mihadarati na kuhakikisha kwamba ahakuna mtoto atakayezaliwa na virusi vya HIV.

Viongozi hao pia wameahidi kuongeza uwezekano wa watu kupata dawa za kurefusha maisha yaani ARV's na kufikia watu bilioni 15.

Na mwisho wanataka kupunguza vifo vitokanavyo na kifua kikuu kwa asilimia 50 ifikapo 2015. Na kila serikali imepewa jukumu la kuhakikisha ina mikakati ya kitaifa, je Kenya ina mikakati gani? na imefikia wapi katika vita hivyo? Alice Kariuki amezungumza na Profesa Aloyce Orago kutoka nchini humo

(MAHOJIANO NA PROFESA ORAGO)