Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dr wa hospitali inayoungwa mkono na UM DR Congo apata tuzo

Dr wa hospitali inayoungwa mkono na UM DR Congo apata tuzo

Pakua

Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametunukiwa tuzo ya kiamataifa na ufalme wa Ubelgiji mwezi Mai mwaka huu kwa mchango wake katika jamii.

Tuzo hiyo ya kimataifa ambayo hutolewa kila baada ya miaka miwili humuendea mtu ambaye amechangia kwa kila hali kuendeleza maendeleo duniani.

Hospitali ya Panzi Bukavu imejikita katika kuwasaidia wanawake wanaokabiliwa na ukatili na hussani waliobakwa, inawapokea, kuwalisha, kuwatibu, kuwapa ushauri nasaha na kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida.

Mwandhishi habari wa kujitolea wa Umoja wa mataifa Mseke Dide amefuunga safari hadi Bukavu na kukutna na Dr Mkwege ambaye anamfafanulia kuhusu tuzo aliyopewa ,nini alichokifanya kustahili tuzo hiyo na thamani yake kwa jamii nay eye binafsi.

(MAHOJIANO NA DR MUKWEGE)