Hamasika
Makala
Mambo 5 ya mkutano wa UN kuhusu Bahari
Kutotupa taka: Mabaki ya samaki yageuzwa chakula cha mbwa
"Kwa pamoja tukidhi mahitaji ya kutunza bahari yetu", Wasihi wenyeji wenza
Habari mpya
Pata Habari za Mkutano kuhusu Bahari
Je wajua
Ukubwa wa bahari ni asilimia 70 ya eneo lote la uso wa dunia, na ni makazi ya takribani asilimia 80 ya viumbe vya dunia? Ni eneo kubwa zaidi la eneo chini ya anga.
Kijarida
Kuhusu Mkutano
Mkutano wa UN kuhusu Bahari
Mkutano kuhusu Bahari unaoandaliwa kwa pamoja na serikali za Kenya na Ureno, unafanyika wakati muhimu kwa kuwa dunia inasaka majawabu ya kutatua matatizo yaliyoota mizizi na ambayo yameibuliwa na janga la COVID-19, majawabu ambayo yatahitaji marekebisho makubwa ya kimuundo na suluhu za pamoja zinazozingatia SDGs. Kuchagiza hatua hizo, Mkutano wa Bahari unasaka kuchagiza kasi ya suluhu bunifu za kisayansi zinazohitajika kwa lengo la kufungua ukurasa mpya wa hatua za kimataifa kwa ajili ya bahari.
Maisha chini ya maji
Bahari ni kitu maarufu kwenye sayari, ikifunika tarkibani theluthi 3 ya Dunia na ni muhimu kwa uhai wa sahari hii. Kama ambavyo mtu hawezi kuishi bila kuwa na mapafu yenye afya, vivyo hivyo Dunia haiwezi kuwa hai bila bahari yenye afya. Bahari ni mapafu ya dunia, ikizalisha hewa ya oksijeni kwa ajili ya uhai na kufyonza hewa ya ukaa na taka. Bahari inahifadhi na kufyonza hewa ya ukaa kutoka duniani, ilhali mimea ya baharini inazalisha oksijeni inayohitajika kwa ajili ya uhai.