Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

UN News Kiswahili

Neno la wiki: Mtambuka

Katika Neno la Wiki hii leo tunaangazia neno “Mtambuka” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema ili kupata maana ya neno Mtambuka, lazima tuachambue maana ya neno "Tambuka", ungane naye upate huo uchambuzi, kisha upate kufahamu maana ya Mtambuka..

Sauti
49"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Mkumbizi

Katika Neno la Wiki hii leo tunaangazia neno “Mkumbizi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. 

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja, kwanza mtu anayesafisha mahali na kuondoa takataka, watu wengi wanamuita mfanyakazi lakini neno sahihi ni Mkumbizi.  Pili ni mtu afuataye wavunaji shambani na kuokota mavuno yaliyosalia kwa bahati na kutumia kama chakula chake.

Sauti
48"
UN News Kiswahili

Neno la wiki: Yamini

Katika Neno la Wiki hii leo tunaangazia neno “Yamini” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.  Bwana Sigalla anasema neno "Yamini" lina maana zaidi ya moja, Mosi, yamini ni kiapo, pili, yamini ni mkono wa mtu wa upande wa kulia au mkono wa kuume na yamini pia ni ahadi aitoayo mtu ya kutenda haki au kuficha siri baada ya kupewa wadhifa fulani..

Sauti
39"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki- Treni na SGR (Standard Gauge Railway)

Katika Neno la Wiki hii leo tunaangazia maneno mawili, moja ni treni ambalo linafahamika sana na pili ni tafsiri ya neno Standard Gauge Railway au SGR ambalo limeshika kasi sasa ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na ujenzi wa reli hiyo unaoendelea hivi sasa. Mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, mhariri mwandamizi katika Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.

Yeye anasema SDR kwa kiswahili sanifu tuite reli ya kisasa.

Sauti
1'6"
UN News Kiswahili

Neno la wiki - Bumbuwazi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Bumbuwazi". Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA . 

Bwana Nuhu anasema unapopigwa na butwaa ama kupatwa na mshangao, hadi ukawa huwezi kuongea hata neno moja basi utakuwa umepigwa na bumbuwazi.

Sauti
13"
UN News Kiswahili

Wafahamu maana ya neno Mlaso? Ungana na Onni Sigalla

Wiki hii tunaangazia neno “Mlaso” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema Mlaso ni aina ya chakula kinachoandaliwa mama ambaye amejifungua ili aweze kuwa na maziwa ya kutosha na kurudisha afya yake.  Maeneo mengine huchanganya chakula hicho aghalabu na damu au maziwa.

Sauti
32"