Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Aghalabu

Katika kujifunza Kiswahili, Mchambuzi Onni Sigalla wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania “BAKITA” anachambua maana na matumizi ya neno “AGHALABU” ambapo anaeleza maana mbili za neno hilo. Tofauti na ile iliyozoeleka kwa matumizi ambapo neno aghalabu hutumiwa kueleza utokeaji wa mara kwa mara wa jambo, mtaalam huyo ameongeza maana nyingine isiyofahamika sana inayohusishwa na kundi la watu katika jamii au jumuiya.

Sauti
1'1"
UN News Kiswahili

NENO LA WIKI: Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto

Neno la wiki limejikita katika kuichambua methali isema, 'Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto'.  Mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora anasema methali hii kimsingi inaeleza dhana ya kuwa ikiwa mtu ana mazoea fulani au kazoea mazingira fulani, hayamtishi, atatekeleza analolitekeleza bila kuogopa.

Sauti
32"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki-Matumizi ya neno AFADHALI.

Aida Mutenyo, mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anachambua matumizi ya neno TAFADHALI.  Anasema kuwa nchini Uganda neno hili ni moja ya maneno yanayowasumbua wazungumzaji wa kiswahili kwani wanalichanganya na neno AFADHALI.

Sauti
1'48"
UN News Kiswahili

Neno La Wiki- Asilani

Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa  baraza la  Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na  anafafanua matumizi ya neno Asilani.

Sauti
55"
UN News Kiswahili

Methali: Kizuri hakikosi ila

Katika NENO LA WIKI hii leo mchambuzi wetu Ken Walibora, mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA anachambua methali Kizuri hakikosi ila. Walibora anasema katika jamii yoyote ile hata kama mtu awe mzuri namna gani lazima ana kasoro na ndipo matumizi ya neno ila.

Sauti
58"
UN News Kiswahili

NENO LA WIKI-KUFA na KUFARIKI

Na sasa ni neno la wiki ambapo Bi. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anachambua maneno KUFA na KUFARIKI. Bi. Mwanahija anasema kwa kawaida kufa linaweza kutumika kwa mnyama au binadamu. Hata hivyo kufariki ni kwa binadamu peke yake na inapendeza zaidi tukisema kufariki dunia.

Sauti
1'
UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Meza

Katika Neno la Wiki linachambuliwa neno MEZA.

Na mchambuzi wetu kwa leo ni Aidah Mutenyo Mwenyekiti wa idara za kiswahili katika vyuovikuu Afrika Mashariki

Sauti
1'22"