Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/UN0159224/Naftalin

Hatuna namna ya kupunguza vifo vya watoto wachanga na wazazi  tukiwaweka pembeni wauguzi wakunga- Amir Batenga

Kupitia mfululizo wa makala za Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambazo zinaangazia wakunga na wauguzi katika mwaka huu wa 2020 ambao umetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama mwaka wa kuwaenzi wauguzi na wakunga, Amir Batenga wa UNFPA Simiyu akitekeleza mradi wa kusaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga na wanawake, mkoani Simiyu Tanzania  kupitia makala hii anamweleza Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Dar es Salaam nchini Tanzania namna ambavyo UNFPA imesaidia kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga kutokana na ushirikiano na wauguzi na wakunga.

Sauti
3'29"
UN

UNFPA na harakati zake za kuhakikisha huduma ya afya ya uzazi kambini

Wakati mkimbizi anajikuta ukimbizini, mahitaji yake yanakuwa ni mengi lakini kwa mazingira aliyonayo anajikuta akitegemea msaada wa kibinadamu kutoka mashirika. Mara nyingi hutokea kwamba mahitaji ambayo yanapewa kipaumbele ni yale ya msingi ikiwemo maji, chakula na huduma za kujisafi. Hata hivyo huduma ya afya na hususan afya ya uzazi inakuwa ni moja ya mahitaji muhimu hususan kwa mama na mtoto.

Audio Duration
6'25"
UNICEF/UN0159224/Naftalin

UNFPA imesaidia sana kuboresha huduma za afya ya uzazi visiwani Zanzibar- Azzah Amin Nofli

Kupitia mfululizo wa makala za Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambazo zinaangazia wakunga na wauguzi katika mwaka huu wa 2020 ambao umetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama mwaka wa kuwaenzi wauguzi na wakunga, Azzah Amin Nofli Afisa programu wa afya ya uzazi, Ofisi ndogo wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia idadi ya watu, ofisi ndogo ya Zanzibar.

Sauti
3'55"
UNICEF/UMichele Sibiloni

Pesa ni muhimu, lakini kwangu mimi, muhimu zaidi ni afya ya mtu- Francis Maina

Kijana Francis Maina ni mwanafunzi wa Chuo cha uuguzi cha St. Regina kilichoko maeneo ya magharibi mwa nchi ya Uganda. Kijana huyu anasema kuwa pamoja na kwamba anasomea kazi ambayo mara nyingi malipo yake ni kidogo, yeye yuko tayari kuifanya kazi hiyo katika hali yoyote kwani furaha yake ni kuona mgonjwa wake akipata huduma nzuri na kisha suala la maslahi litafuata baadaye.

Sauti
3'33"
© UNICEF/Thomas Nybo

Jamii ya sasa wana imani zaidi na hospital kuliko wakunga wa jadi-Mkunga wa jadi

Kwa miaka mingi kabla ya ukuaji wa teknolojia na hata baada ya kuanzishwa hospitali za kisasa, jamii nyingi ziliendelea kuwatumia wakunga wa jadi kuwasaidia akina mama wajawazito kujifungua hususani kwa wale walikuwa mbali na huduma za kiafya. Bi Rehema Muhando wa kijiji cha Mwera huko Pangani Tanga Tanzania anasema ameifanya kazi ya ukunga kwa miaka mingi na anajivunia kuwa watoto wengi wamepita mikononi mwake. Lakini anasema hivi sasa, jamii imebadilika sana. 

Sauti
6'5"
UN /MINUSCA

Jamii yetu imenufaika sana na matangazo ya redio za kijamii.

Ikiwa leo ni siku ya redio duniani ambapo ulimwengu unakiangazia chombo hicho ambacho kwa miongo mingi kimekuwa muhimu kupitisha taarifa muhimu kwenda kwa jamii na pia kuwapa wanajamii fursa ya kueleza mawazo yao katika ujenzi wa maisha yao, Umoja wa Mataifa umeamua maadhimisho ya mwaka huu yalenge kuzienzi redio za kijamii ambazo zinatoa fursa kwa watu walioko mashinani.

Sauti
3'28"
© UNICEF

Huduma tunazozitoa sisi wauguzi zimepunguza sana magonjwa Pangani

Kazi ya uuguzi ina panda shuka zake kama zilivyo kazi nyingine lakini kinachotufanya tuendelee kusonga mbele ni pale tunapoona watu wamepona na wameelimika kuhusu afya zao. Ni kauli ya Vailet Prosper ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu katika Hospitali ya Pangani mkoani Tanga Tanzania. Vailet anafanya kazi ya uuguzi na ukunga ambayo mwaka huu inaenziwa na shirika la afya duniani WHO kuwa ni miongoni mwa kazi muhimu katika ustawi wa afya ya binadamu ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo endelevu.

Sauti
3'55"
UNFPA Mozambique

Mwanafunzi wa uuguzi ahidi kuhudumu kwa dhati akianza kazi, Uganda

Miti michanga ndio huleta uhakika wa uendelevu wa msitu. Sawa na hivyo, wanafunzi wa ukunga ndio uhakika wa uwepowa huduma yao kesho na baadaye. Kuendelea na msururu wa makala yetu kuhusu wauguzi na wakunga mwaka huu, tuelekee nchini Uganda ambapo John Kibego amezungumuza na mwanafunzi Cyrus Kanzike wa chuo cha wauguzi na wakunga cha Hoima School of Nursing and Midwifery mjini Hoima. Kijana huyo anaeleza sababu zilizomsukumiza kuamua kusomea ukunga ikiwemo kifo cha nyanya yake katika maumimu kakubwa baada ya kuugua kiharusi.

Sauti
3'40"
UNICEF/Catherine Ntabadde

Manusura wa ukeketaji na juhudi za kuwaokoa wasichana kuepukana na uovu huo Tanzania

Dunia imeendelea kupambana na ukatili mkubwa wanaofanyiwa wasichana na wanawake lilikwemo suala la ukeketaji ambapo sehemu ya kiungo cha uzazi cha mwanamke aghalabu wasichana wa umri mdogo hukatwa kutokana na imani za mila. Manusura Robi Samuel huko Tanzania ni mmoja wa watu ambao wamekuwa jasiri wa kuweka wazi kuwa wamekeketwa na sasa anapambana kuhakikisha hakuna mtoto mwingine wa kike anayekumbana na madhila haya. Warren Bright, Afisa Mkuu wa mawasiliano wa UNFPA Tanzania, amezungumza na Robi katika Makala hii ya kuelimisha.

Sauti
6'1"