Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN SDGs

Ninaitekeleza ndoto yangu ya kufanya kazi na Umoja wa Mataifa kwa kuwafundisha watoto kuhusu Umoja huo

Mwalimu Joseph Gichana akiwa kijana alikuwa na ndoto ya kufanya kazi na Umoja wa Mataifa. Ingawa ndoto hiyo bado haijatimia, hivi sasa jwa kipindi hiki akifundisha masomo ya uchumi nchini China ameamua kuwaelimisha wanafunzi wake kuhusu malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs kama mchango wake wa kufanikisha ndoto yake na kusaidia kazi za Umoja wa Mataifa. Je anafanikiwa? Katika mahojiano yake na Flora Nducha mjini New York Marekani, Mwalimu huyo mzaliwa wa Kenya anaeleza kinaga ubaga.

Sauti
3'33"
Picha/Siegfried Modola

Mkimbizi kutoka Burundi akiwa kambini Kakuma atumia muziki kubadilisha maisha yake 

Alipoondoka nchini Burundi akiandamana na dada yake mwaka 2009,  msichana Azam Zabimana alikuwa na umri wa miaka 15. Kutokana na taabu na dhiki walizokuwa wanapitia nchini Burundi baada ya kuwapoteza wazazi wao, wasichana hawa walipata msamaria mwema aliyewasafirisha hadi mjini Nairobi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR lilipata kuwahamisha hadi kambi ya Kakuma.Licha ya wao kupitia hali ngumu Azam alijibidiisha na kuwa msanii ambapo hadi sasa amefanikiwa kutunga na kurekodi takriban nyimbo sita.

Sauti
3'48"

Kaunti ya Makueni nchini Kenya tumeweka mikakati mingi kumkomboa mwanamke-Mwau

Mwanamke mashinani anakabiliwa na changamoto mbalimbali iwe ni masuala ya afya, maji au hata ukiukwaji wa haki zake. Kwa kutambua changamoto ambazo zinawakabili wanawake na katika juhudi za kufanikisha lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030, serikali ya kaunti ya Makueni mashariki mwa Kenya imeweka mikakati mbali mbali ili kufanikisha ustawi wa mwanamke, katika makala hii, Grace Kaneiya amezungumza na Adelina Mwau, Naibu gavana wa kaunti ya Makueni ambaye amemwelezea yale wanayoyafanya kumuinua mwanamke, ungana nao.

Sauti
3'14"
© UNHCR/Diana Diaz

Adhabu ya wanafunzi shuleni yazua mjadala kutoka kwa wahusika Tanzania

Upatikanaji wa elimu ni suala ambalo linaghubikwa na changamoto nyingi iwe ni kwa upande wa kufikia elimu yenyewe au pale elimu inapopatikana viwango vyake au mazingira yanayokwamisha ufikiaji wa elimu hiyo. Suala la nidhamu pia na dhamira ya wanafunzi katika kupata elimu pia ni mtihani. Hali ni kama hiyo kwa wazazi wa wanafunzi wa shule moja nchini Tanzania kama anavyosimulia John Kabambala wa Radio washirika Kids Time FM ya mkoani Morogoro nchini humo.

Audio Duration
3'31"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Muziki wangu siyo wa biashara bali ni kuhamasisha jamii yangu katika masula mbalimbali-Kala Jeremiah

Ziko namna mbalimbali za kushiriki katika utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, yaliyopangwa kuwa yametekelezwa ifikapo mwaka 2030. Kwa upande wa mwanamuziki kijana Kala Jeremiah kutoka Tanzania ambaye pia ni Balozi wa vijana nchini humo, njia ya muziki ndiyo aliyoamua kuitumia kufikisha ujumbe kwa jamii.

Sauti
3'41"
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya

Uwepo wa wanawake uongozini umeleta matokeo chanya Kenya- Shebesh

Uwepo wa wanawake katika nafasi za uongozi umezaa matunda na matokeo yake ni dhahiri iwe ni kwa upande wa maswala ya mirathi au hata katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu hususan watoto. Kauli hiyo ni ya Rachel Shebesh, Katibu Tawala kwenye wizara ya maswala ya jinsia, wazee na watoto nchini Kenya ambaye katika mahojiano na Flora Nducha mapema mwaka huu kandoni mwa mkutano kuhusu hali ya wanawake amesema ari ya kisiasa ni muhimu katika kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia.

Sauti
3'57"
© UNHCR/Socrates Baltagiannis

Huduma ya kibinadamu ni wito-Wakili Kamunya

Kutoa huduma ya kibinadamu iwe ni katika mazingira yoyote yale ni wito ambao ni lazima utoke moyoni amesema Ann N. Kamunya wakili mtetezi wa haki za wanawake, raia wa Kenya ambaye sasa yuko Ankara, Uturuki akifanya kazi za huduma za kibinadamu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Sauti
6'8"
UNICEF/Tapash Paul

Mapendekezo ya UNICEF Tanzania katika kuimarisha elimu ya awali

Hii leo katika makala tunaendelea na sehemu ya pili ya mahojiano kati ya Stellla Vuzo wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na Audast Muhinda, afisa kitengo cha elimu katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF ambapo Bwana Muhinda anatoa mapendekezo yake katika kuhakikisha kwamba idadi ya watoto wanaopokea elimu ya awali inaongezeka.

Sauti
3'50"
AU-UN IST/Stuart Price

Biashara ya fedha za kigeni mtandaoni yamwinua kijana mmoja nchini Kenya

Akiwa mwanafunzi chuoni nchini Kenya, Paul Mugenda alikuwa na changamoto kubwa za karo hali iliyosababisha  aanze kufanya biashara ndogo ndogo kujikimu chuoni. Hata hivyo siku moja alikutana na mtu aliyemshauri ajaribu biashara ya ununuzi na uuzaji wa fedha za kigeni kwa njia ya kieletroniki ikimaanisha kuwa teknolojia ya mtandao na taarifa za fedha ndio vilikuwa muarobaini kwa shida yake.

Sauti
4'24"