Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapendekezo ya UNICEF Tanzania katika kuimarisha elimu ya awali

Mapendekezo ya UNICEF Tanzania katika kuimarisha elimu ya awali

Pakua

Hii leo katika makala tunaendelea na sehemu ya pili ya mahojiano kati ya Stellla Vuzo wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na Audast Muhinda, afisa kitengo cha elimu katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF ambapo Bwana Muhinda anatoa mapendekezo yake katika kuhakikisha kwamba idadi ya watoto wanaopokea elimu ya awali inaongezeka.

Hii ni kufuatia ripoti ya mapema mwaka huu ya UNICEF ambayo imesema elimu ya awali ni msingi muhimu ambapo elimu ya baadaye inategemea kwa kiasi kikubwa mafanikio ya elimu hiyo. Hata hivyo watoto wengi duniani kote wanakosa fursa hiyo muhimu na hivyo kuongeza hatari ya kurudia madarasa au hata kutoendelea na masomo na hivyo kuwatenganisha na wanafunzi wenzao ambao wao walihudhuria.

Kwanza bwana Muhinda anaanza kwa kutoa mapendekezo yake kuhusu kuinua ubora wa elimu ya awali.

Audio Credit
Stella Vuzo
Sauti
3'50"
Photo Credit
UNICEF/Tapash Paul