Vituo vya kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya ni msaada mkubwa
Hii leo ikiwa ni siku ya kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya duniani, vituo vya kusaidia waathirika wa madawa hayo vimekuwa msaada mkubwa wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasema ya kwamba watu milioni 35 ulimwenguni kote wana matatizo yatokanayo na matumizi ya madawa hayo ilhali ni mtu 1 tu kati ya 7 ndiye anayepata matibabu. Assumpta Massoi na ripoti kamili.