Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapiganaji wa zamani 126 wa Al-Shabaab walihitimu uanagenzi

Wapiganaji wa zamani 126 wa Al-Shabaab walihitimu uanagenzi

Pakua

Ukosefu wa amani na usalama nchini Somalia, umekuwa chanzo cha vifo na ukimbizi kwa wananchi iwe ndani  ya nchi yao au nje ya nchi huku kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kikiwa mara kwa mara kikijinasibu kushiriki kwenye mashambulizi hususan kwenye mji mkuu Mogadishu. 

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la uhamiaji, IOM pamoja na ujumbe wake Umoja huo nchini Somalia UNSOM wamechuka hatua kuwanasua vijana kwa kuanzisha na kufadhili programu ya kuwawezesha vijana hao waliojisalimisha kutoka kundi la wanamgambo la Al-Ashabaab kupata stadi mbalimbali ili hatimaye warejee katika jamii na kuweza kujipatia kipato.

Je ni nini kinafanyika? katika makala hii Patrick Newman anafuatilia kilichofanyika kwenye jimbo la kusini maghribi 

Audio Duration
2'52"
Photo Credit
UN Photo/Stuart Price