Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msichana mwenye umri wa miaka 16 nchini Tanzania atengeneza Apu ya kusaidia wanawake wajawazito kufuatilia hali zao.

Msichana mwenye umri wa miaka 16 nchini Tanzania atengeneza Apu ya kusaidia wanawake wajawazito kufuatilia hali zao.

Nchini Tanzaniamsichana Khatija Safi Juma mwenye umri wa miaka 16 amebuni apu ya kusaidia wanawake wajawazito kukumbuka kwenda kupata huduma ya kliniki, wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa vijana kuwa wabunifu kusaka suluhu za changamoto kwenye jamii zao.

Khatija anayesoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Ndono wilayani Uyui, Tabora nchini Tanzania amesema msingi wa kubuni apu hiyo ni..

(Sauti ya Khatifa Safi Juma)

“Ni kutokana na maeneo ambayo tunaishi, na kuona kwamba akina mama wengi wanapata shida pale wanapokuwa wajawazito kwa kuwa hospital ziko mbali. Lakini pia kutokana na kutokuwa na uelewa zaidi kuhusu masuala ya afya, hicho ndicho kimenipelekea kubuni hiyo App. Na hiyo alianza tangu nilipoingia kidato cha kwanza kwani ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuishi vijijini na kushuhudia vifo.”

Na kuhusu ni namna gani ‘App’ hiyo inafanya kazi, Khatija anafafanua,

(Sauti ya Khatifa Safi Juma)

“Ina sehemu ambayo inahifadhi taarifa za mwanamke kama ni mjamzito kuhusu ujauzito wake na hapo kutakuwa na sehemu ambayo inamkumbusha kuhusu tarehe za kwenda kliniki, lakini pia kuna sehemu za ushauri kwa akina mama kwa ujumla. Kuna pia vyakula anavyotakiwa kula na pia tumeandika athari zipi unaweza kuzipata usipoenda kliniki au kutofuata mlo ipasavyo, hivyo ndivyo tumeziweka.”

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, katika masomo ya ngazi ya juu takribani asilimia 30 pekee ya wanafunzi wa kike ndiyo wanachagua masomo yanayohusiana na sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati. Vile vile takwimu hizo zinabainisha kuwa wanawake watafiti  ni asilimia 30 pekee kote duniani.

Pakua

Nchini Tanzania msichana Khatija Safi Juma mwenye umri wa miaka 16 amebuni apu ya kusaidia wanawake wajawazito kukumbuka kwenda kupata huduma ya kliniki, wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa vijana kuwa wabunifu kusaka suluhu za changamoto kwenye jamii zao.

 

Audio Credit
Arnold Kayanda/Khatija safi Juma/Malongo Mbeho
Sauti
5'27"
Photo Credit
UNICEF/Iana Creul