Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka ufuatiliaji na tahadhari Afrika wakati aina mpya ya COVID-19 imeibuka

Majaribio yanaonesha kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona ina uwezo mkubwa wa kuzuia hatariza COVID-19.
University of Oxford/John Cairns
Majaribio yanaonesha kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona ina uwezo mkubwa wa kuzuia hatariza COVID-19.

WHO yataka ufuatiliaji na tahadhari Afrika wakati aina mpya ya COVID-19 imeibuka

Afya

Wakati hivi karibuni kumeibuka aina mpya ya virusi vya corona au COVID-19 barani Afrika ambavyo kiwango cha maambukizi yake ni cha juu zaidi, shirika la afya duniani WHO leo limetoa wito kwa nchi zote za bara hilo kuongeza kiwango cha ufuatiliaji na tathimini kupitia mtandao wa maabara Afrika ili kubaini mwenendo wowote mpya wa maambukizi na kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko huo.

Kwa mujibu wa shirika hilo Afrika Kusini hivi karibuni imebaini aina mpya ya virusi ambavyo ni SARS-CoV-2 ambavyo vinaonekana kuambukiza kwa urahisi Zaidi na kuna uwezekano vinahusiana na virusi vya mlipuko wa sasa wa coronavirus">COVID-19 unaoendelea nchini humo.

Hata hivyo tathimini zaidi inaendelea ili kujua umuhimu kamili wa mabadiliko ya ugonjwa huo.

Nigeria pia inafanya uchunguzi zaidi wa vitrusi hivyo vipya vilivyobainika katika sampuli zilizokusanywa mwezi Agosti na Oktoba.

Wanafunzi wa Mauritania waliporejea shuleni baada ya miezi kadhaa ya shule kufungwa kutokana na COVID-19
© UNICEF/Raphael Pouget
Wanafunzi wa Mauritania waliporejea shuleni baada ya miezi kadhaa ya shule kufungwa kutokana na COVID-19

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti“Kuzuka kwa aina mpya ya virusi vya COVID-19 sio kitu kigeni. Hata hivyo wale walio na kiwango cha kasi cha maambukizi au wenye uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi hayo ndilo suala linalotia hofu. Chunguzi muhimu na za kina zinaendelea ili kuelewa kikamilifu tabia ya aina hiyo mpya ya virusi na kuchukua hatua zinazostahili.”

Mwezi Septemba 2020, WHO na kituo cha Afrika cha kuzuia na kudhibiti magonjwa CDC walizindua mtandao wa maabara 12 barani Afrika ili kusisitiza ufuatiliani na kubaini virusi hivyo vipys vya SARS-CoV-2.

Tangu Desemba 23 mlolongo wa sampuli 4948 umeshatengenezwa katika ukanda huo wa afrika ukiwakilisha asilimia 2% tu ya sampuili 295,101 zilizofanyika duniani kote hadi sasa.

Afrika Kusini ambayo imefanya ufuatiliaji mkubwa zaidi wa idadi hiyo imebaini imebaini vinasaba 35 vya virusi hivyo SARS-CoV-2 na Nigeria vinasaba 18.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moet.
UN News/Video capture
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moet.

Kuviweka kwenye kundi virusi kutoka nchi tofauti vyenye vinasaba vinavyofanana inaonyeshja uhusiano au uingiaji wa virusi hivyo kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Ofisi ya WHO Afrika inatoa mwuongozo wa msaada wa kiufundi na kukusanya msaada wa kifedha kwa ajili ya kuongeza kasi ya kukusanya sampuli katika nchi nyingi za ukanda huo pamoja na kusaidia kusafirisha sampuli hizo kwenye maabara maalum kutoka nchi ambazo hazina vifaa maalum vya upimaji.

Bi. Moeti ameongeza kuwa “Ingawa ufuatiliaji na kubaini COVID-19 ni kipengele muhimu cha kukabiliana na janga hilo, hatua za kiafya za umma kama vile kunawa mikono, kujitenga umbali baina ya mt una mt una kuvaa barakoa bado vinasalia kuwa muhimu katika kudhibiti maambukizi. Hatua za sasa za kuzuia maambukizi bado zinafanyakazi hata kwa aina hii mpya ya virusi ya SARS-CoV-2”.

Janga la COVID-19 imeweka mazingira yanayofanya watu waliohatarini kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
© UNICEF/Michele Sibiloni
Janga la COVID-19 imeweka mazingira yanayofanya watu waliohatarini kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.

Aina hii mpya ya virusi imezuka wakati maambukizi ya COVID-19 bado yanaendelea kuongezeka katika nchi 47 za ukanda wa WHO Afrika yakikribia kufikia kilele kilichoshuhudfiwa mwezi Julai.

Katika siku 28 zilizopita, Algeria, Botswana, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Ethiopia, Kenya, Namibia, Nigeria, Afrika Kusini na Uganda zimearifu idadi ya juu zaidi ya maambukizi mapya yakiwa ni jumla ya asilimia 90% ya maambukizi yote ukanda huo.