Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa kila siku inayopita, athari za janga la COVID-19 na matokeo yake ni dhahiri :UNFPA

UNFPA imekuwa ikiwasaidia wanawake wajawazito Darfur Magharibi kufuatia kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu katika eneo hilo.
UNFPA
UNFPA imekuwa ikiwasaidia wanawake wajawazito Darfur Magharibi kufuatia kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu katika eneo hilo.

Kwa kila siku inayopita, athari za janga la COVID-19 na matokeo yake ni dhahiri :UNFPA

Afya

  Kwa kila siku inayopita, athariza janga la COVID-19 na matokeo yake ni dhahiri :UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA , limesema linashikamana na wale wote wanaojitolea na kuwa katika mstari wa mbele kupigana na janga la virusi vya corona au COVID-19: kuanzia kwa wahudumu wa afya na wanaojitolea kusaidia bila malipo. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA , limesema linashikamana na wale wote wanaojitolea na kuwa katika mstari wa mbele kupigana na janga la virusi vya corona au COVID-19: kuanzia kwa wahudumu wa afya na wanaojitolea kusaidia bila malipo. 

kwa ujasiri kuwatunza wagonjwa, kwa madereva wa mabasi na wafanyikazi walio kwenye mstari wa mbele wa kupigana na janga hili. Na kuomboleza na wale ambao  wamepoteza wapendwao katika janga hii kubwa zaidi la kiafya katika karne hii.

 

Wanawake hawa zamani walikuwa mangariba, sasa wamedondosha nyembe na wanashiriki katika ukeketaji mbadala kufuatia mafunzo kwenye kituo cha Masanga mkoani Mara. Kituo hiki kinapata msaada kutoka shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA. Maghariba pia wakid
Warren Bright/UNFPA Tanzania
Wanawake hawa zamani walikuwa mangariba, sasa wamedondosha nyembe na wanashiriki katika ukeketaji mbadala kufuatia mafunzo kwenye kituo cha Masanga mkoani Mara. Kituo hiki kinapata msaada kutoka shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA. Maghariba pia wakidondosha nyembe wanakuwa na mradi mbadala wa kupata kipato.

 

COVID-19 imeleta mtihani kwa  jamii ya kimataifa lakini bado UNFPA  inafanya kazi na serikali, washirika, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafadhili  na inajiandaa kupigana na janga hili. Mipango ya kuendeleza biashara  iko katika mstari wa mbele, na kujitolea kwa hali na mali kuwahudumia wasiojiweza.

Kama ilivyo kwa majanga mengi , janga hili limesumbua sana upatikanaji wa huduma za uzazi ,maisha na huduma za afya ya uzazi na uwezo wa kuzingatia dhuluma za kijinsia wakati wanawake na wasichana wanahitaji huduma hizi zaidi. UNFPA inafanya kazi na serikali na washirika wa kuweka kipaumbele katika mahitaji maalum ya wanawake na wasichana .

Sambamba na malengo yetu yakutimiza hitaji la kawaida la uzazi wa mpango, kutimizwa kwa uzazi wa mpango kunaweza kuzuia vifo wakati wa uzazi  na kumaliza ukatili wa kijinsia na ukatili mwingine ifikapo 2030.

UNFPA inatoa wito kwa wafadhili kufadhili nchi zinazoendelea ili  kuweza kupambana na virusi vya COVID-19. Mifumo dhaifu ya afya ya umma na msaada wa kijamii, pamoja na nchi dhaifu zilizoghubikwa na changamoto za kibinadamu, zinahitaji dola  185 kuweza wasaidia kugharamia gharama huduma muhimu za kiafya.

Uzazi wa mpango
UNFPA
Uzazi wa mpango

 

Ombi hilo la UNFPA litazingatia kuimarisha mifumo ya afya, ununuzi na ufikishaji wa vifaa muhimu, kulinda wafanyakazi wa huduma za afya, na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za   afya ya uzazi. Pia huduma za kuwasaidia waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia na  kuelimisha juu ya hatari ya COVID-19  na ushiriki wa jamii.

UNFPA inasisitiza kwamba sasa ni wakati wa mshikamano, ha hatupaswi kusahau kuwa kuna watu ambao labda hatuwezi kuwaona, ambao wako kwenye hatari kubwa kwa sababu ya janga hili la Corona.

Mfano wanawake wajawazito, ambao wanahitaji kulindwa, lakini hawana uhakika kama ni salama kwenda kliniki. Wanawake katika mahusiano yaliyoghubikwa na dhuluma ambao sasa wanalazimika kusalia nyumbani na wadhuumu wao na wanahofia usalama wao.

Mamilioni ya watu katika kambi za wakimbizi, ambao wanahesabu siku kabla corona  iwafikie,kwa sababu  kujiepusha na mrundikano wa watu kwao sio  chaguo. Wazee, ambao wengi wao wametengwa na ambao wana hatari kubwa ya kuwa wagonjwa sana kutokana na virusi hivi

 

Mwanamke huyu zamani alikuwa ngariba, sasa amedondosha wembe na anashiriki katika ukeketaji mbadala kufuatia mafunzo kwenye kituo cha Masanga mkoani Mara. Kituo hiki kinapata msaada kutoka shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA. Maghariba pia wakidondosh
Warren Bright/UNFPA Tanzania
Mwanamke huyu zamani alikuwa ngariba, sasa amedondosha wembe na anashiriki katika ukeketaji mbadala kufuatia mafunzo kwenye kituo cha Masanga mkoani Mara. Kituo hiki kinapata msaada kutoka shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA. Maghariba pia wakidondosha nyembe wanakuwa na mradi mbadala wa kupata kipato.

 

UNFPA inatoa msaada wa vifaa kwa mifumo iliyoathirika ya afya na kulinda afya ya wauguzi na wakunga. Kwa mfano Uchina, Iran na Ufilipino imegawa vifaa vya kuzingatia usafi muhimu na vitu vingine kwa walio hatarini zaidi na kinga ya kibinafsi, na vifaa kwa wahudumu wa afya. Na huko Moldova wamezindua ukurasa mtandaoni kwa ajili ya mfumo wa afya ambao unaonyesha dhana ya sasa, iliyogawanywakwa kuzingatia eneo, jinsia, umri na hali ya ujauzito.

 Lakini shirika hilo linasema linahitaji kufanya mengi zaidi kuhakikisha kwamba mahitaji ya karibu na  muhimu zaidi ya wanawake na wasichana wa ulimwengu yametimizwa  wakati tunapambana na janga la  COVID-19 na wakati wa changamoto za miezi ijayo.

Kwa mujibu wa shirika la UNFPA, Janga hili la kimataifa linahitaji suluhu ya kimataifa . Limeisihi jamii ya kimataifa  kusaidia wale wote walioathiriwa najanga hili, wale wote walio na COVID-19 na wale ambao wametengwa, na kuyimwa huduma wanazohitaji. "Tafadhali ungana nasi katika kupigania afya ya wanawake na wasichana wakati wakati huu ambao wanatuhitaji sana."